MTANDAO wa mashirika ya wafugaji Tanzania
(Tanzania Pastoralist Community Forum)umelaani vitendo vya ukatili na ukiukaji
wa haki za binadamu ,unaofanywa katika operationi tokomeza
Majangili inayoendeshwa na serikali kwa lengo la kutokomeza ujangili
dhidi ya wanyama pori
Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari wadau hao wamedai kuwa zoezi hilo limejaa matukio
ya kusikitisha na ya kudhalilisha wananchi pia
limesababaisha mamia ya watu kukimbia makazi yao kwa hofu ya kukamatwa.
Mratibu wa mtandao huo Joseph Ole Parsambei amewaambia
waandishi wa habari kuwa operationi hiyo imewatesa watu katika maeneo mbali
mbali nchini na kama serikali haitaaangalia ukiukwaji wa sheria watalazimika
kuiomba mahakama ilisitishe.
Alisema wafuagaji kutoka katika Wilaya za Monduli
,Longido ,Simanjiro na Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wamekuwa
wahanga wakubwa wa vitendo hivyo.
Alifafanua kuwa katika wilaya ya Monduli Kata ya Mswakini,
watu wanne wamekamatwa na kupelekwa kusikojulikana hadi
sasa na wengine kukimbia makazi yao kwa hofu ya kukamatwa
.
Wilaya ya Ngorongoro kijiji cha Ololosokwan watu 13 wamekamatwa
na mifugo yao zaidi ya 2000 inashikiliwa Wilaya ya Serengeti ikiwa ni baada ya
wiki mbili .
Wilaya ya Londido kijiji cha Oromba watu nane wamekamatwa
kwa sababu hizo ,kupigwa na kunyanyaswa .
Katika Wilaya ya Simanjiro watu wawili wamekamatwa na kupigwa
,nyumba zao kuchomwa na moto na Wilaya ya Chunya Ng’ombe 169
zimetaifishwa na mfugaji mmoja aliyetajwa jina la Magaka Ninya aliuwawa
katika zoezi hilo .
Waziri wa mali asili na utalii
Balozi Khamisi Kagasheki alipoulizwa kuhusu madai hayo alikanusha na
kusema kuwa zoezi hilo la kusaka mtandao wa ujangili hapa nchini linaendelea
vizuri.
0 comments:
Post a Comment