Tuesday, December 4, 2012

WIKI, moja baada  ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchikavu (Sumatra) kupokea maoni ya kuongezeka kwa nauli za mabasi yaendayo mikoani kutoka kwa wadau wa usafiri, nauli za mabasi hayo zinadaiwa kuanza kupanda.

Habri   kutoka kwa baadhi ya makarani wa kampuni za mabasi yaendayo  mikoani katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendeyo mikoani Ubungo (UBT), jijini Dar es Salaam zinaelza  kuwa nauli zimeanza kupanda hasa kwa magari yaendayo mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

“Baadhi ya magari yanayokwenda mikoani yameshaanza kuongeza nauli toka Shilingi20, 000 na 22,000 hadi 25,000 kwa magari yaendayo  Arusha na Kilimanjaro.”

Kwa mujibu wa makarani hao  sio mabasi yote  yenye tabia ya kupandisha nauli kiholela hasa katika kipindi cha kuelekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

Hidaya Hassan, karani Kampuni ya Basi ya Tashrif ambayo mabasi yake yanafanya safari kati ya Dar es Salaam na Tanga, alisema nauli zinaweza kupanda kuanzia mwezi huu kwa kuwa kipindi hiki kunakuwapo na idadi kubwa ya abiria wanaotaka kusafiri kwenda mikoani huku idadi ya magari ikiwa ni ndogo.

Shekha Lema, karani Kampuni ya Basi ya Master City Ltd ambayo mabasi yake  yanafanya safari kati ya Dar es Salaam na Mwanza na maeneo mengine, alisema nauli bado hazijaanza kupanda kwani inakuwa vigumu kwao kufanya hivyo kwa kuwa hata vitabu vyenyewe vya risiti vimegongwa muhuri na abiria ni wachache.

“Sisi mabasi ya kampuni yetu yanayofanya safari kati ya Dar na Mwanza, nauli bado ni ile ile ya Sh.35, 400, hatuwezi kuibadilisha,” alisema Lema na kuongeza:

Baadhi ya makarani hao pia, wamedai kuwa upandishwaji holela wa nauli haufanywi na kampuni bali hufanywa na madalali ambao hununua tiketi na kuwauzia abiria kwa bei kubwa na matokeo yake Sumatra inapokagua wanaolaumiwa ni kampuni, jambao ambalo wamesema si kweli.

“Upandishwaji wa nauli kiholela ni kama vile mfumuko wa bei za vitu au bidhaa masokoni. Madalali ndio wanaohusika na upandishaji huo kwa kununua tiketi na kuziuza tena kwa abiria kwa bei kubwa, na wala sio kampuni,” alisema Meneja wa Kampuni ya Mabasi ya Master City Ltd, Miraji Mgongolwa.

Hata hivyo, maelezo ya baadhi ya makarani hao waliokuwa wanadai kutokupanda kwa nauli hizo, kunakinzana na nauli aliyotozwa abiria mmoja aliyekuwa anasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza baada ya kukatiwa tiketi ya Sh. 38,000 tofauti na na ile ya 35,400 iliyotajwa kutozwa na Kampuni ya Master City.

“Naenda Mwanza, nimelipa nauli ya Sh. 38, 000,” alisema Mwita Wilson (25) akiwa UBT muda mfupi baada ya kukata tiketi. Kinyunyu George, Karani wa Kampuni ya Mabasi ya Mapanda, alisema kuwa nauli bado hazijapanda kwani Sumatra wapo wakivinjari kituoni hapo huku wakiwauliza abiria iwapo wametozwa nauli zaidi ya ile iliyopangwa na ma
mlaka

0 comments:

Post a Comment

Time Management

Translator

Popular Posts

Blog Archive

Fellow Bloggers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews