Aliyetangazwa kuwa
askofu mkuu wa kanisa Anglikana Cantebery na ambaye amethibitishwa hii
leo, Justin Welby amesema ameshangazwa sana na wadhifa aliopewa wa
kuliongoza kanisa hilo.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Askofu
Justin Welby ambaye ni askofu wa Durham, alielezea msimamo wake wa
kuunga mkono kutawazwa kwa wanawake kama maaskofu.
Aliongeza kuwa watu watu hawapaswi
kuwanyanyapa wapenzi wa jinsia moja kanisani, lakini akakiri kuna
mgawanyiko kanisani kuhusu ndoa za jinsia moja.
Welby aliyefanya kazi katika sekta ya mafuta ,
anaonekana kama mhafidhina kwa mrengo wa kanisa hilo ambalo linaegemea
upande wa kiivanjelisti.
Ataanza kazi yake mwezi Machi mwaka ujao baada
ya Askfo mkuu Rowan Williams kuachia ngazi.
Baada ya uteuzi wa Askofu mkuu Justin Welby kuwa
mkuu wa Kanisa la Anglikana, viongozi mbalimbali wa kanisa hilo
wamezungumzia uteuzi huo.
Askofu mkuu wa kanisa la Anglikana nchini
Nigeria, Nichola Okoh, ameimbia BBC kuwa uhusiano wa wapenzi wa jinsia
moja usitetewe na Kanisa.
0 comments:
Post a Comment