HOFU YA VITA VYA KIENYEJI NGORONGORO,WAALIMU ,WANAFUNZI WAKIMBIA,
SERIKALI YAAHIDI KUTATUA MZOZO BAINA YA WASONJO NA WAMASAI
Mwandishi wetu Loliondo
WAALIMU
na wanafunzi wa shule ya msingi Nan katika kata ya Engusero Sambu
Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha wamekimbia shule hiyo kutokana na
hofu ya kuvamiwa na kuuawa kwa sialaha za moto zinazodaiwa kumilikiwa na jamii
za kisonjo na kimasai ambazo zimekuwa zikipigana mara kwa mara.
Shule
hiyo ina wanafunzi 248 kati yao wavulana
158 na wasichana 100.
Hivi
karibuni watu wanaodhaniwa kuwa ni vijana wa Kisonjo wakidaiwa na sialaha za moto walivamia
katika eneo hilo na kupora mifugo na kujeruhi watu
kadhaa kwa risasi.
Waalimu
hao ambao hawakutaka kutajwa majina yao waliwaambia waandishi wa
habari kuwa tetesi za morani wa kimasai kuvamia maeneo ya wasonjo kulipiza
kisasi zimezagaa katika eneo hilo na kwa hiyo hawawezi kufanyakazi katika
mazingira hayo.
“Hatutaki
kutaja majina yetu tutapata matatizo ,Hata wanafunzi hawapo tutafanya kazi gani
hapa ,serikali imeshindwa kumaliza migogoro ya jamii hizi na sisi
tunakuwa wahanga”alisema Mwalimu mmoja wa shule hiyo.
Walisema
kuwa hata wanafunzi wa darasa la saba walilazimika kuhamishwa kwenda kufanya
mitihani wa kumaliza elimu ya msingi katika eneo la Wasso kutokana na hali ya
usalama kuwa tete.
“Unajua
katika tukio hilo mtu mmoja aliuawa mashine ya kusaga nafaka kuchomwa moto na
mamia ya mifugo ya wamasai iliporwa na watu hao ambao wanadaiwa kutumia silaha
za kivita ikiwemo AK47 na SMG”alisema mkazi wa Kisangiro
Alieleza
kuwa baadhi ya watoto wamebaki majumbani miezi miwili na kama serikali haitawafuatilia
hiyo ndio itakuwa njia ya wazazi kukwepa jukumu la kuwasomesha.
Naye
afisa elimu shule za msingi Wilayani humo Papaa Kinyi alithibitisha kuwepo kwa
hali na kusema kuwa wanajaribu kuwashawishi waalimu hao kurudi shule kwa kuwa
vyombo vya ulinzi na usalama vinafuatilia hali ya mambo katika eneo hilo
“Ni
kweli Waalimu wana hofu lakini serikali inafanya kila linalowezekana kurejesha
amani katika eneo hilo”alisema Papaa Kinyi.
Mkuu
wa Wilaya ya Ngorongoro Elias Lali alisema kuwa serikali inaendesha zoezi la
kupokonya silaha za moto kutoka kwa watu wanaozimiliki kinyume na sheria.
Alisema
hadi kufikia sasa wamekwisha kamata bunduki mbili aina ya SMG na Riffle na
kwamba zoezi bado linaendelea.
“Ni
kweli hapa kuna hofu kutokana na uvumi unaoendelea lakini vyombo vya usalama
viko tayari kukabili tishio lolote la usalama ,tunajaribu kuhamasisha waalimu
na wazazi kuwarudisha watoto kuendelea na masomo”alisema Lali
Alieleza
kuwa serikali iko mbioni kupeleka msuluhushi wa mipaka ili kumaliza migogoro
yote ya ardhi katika Wilaya hiyo.
"Msuluhishi
huyo atateuliwa na wizara ya ardhi na tunaamini kuwa hili tatizo la mipaka
likishughulikiwa vizuri hii migogogro na vita vitaisha hapa"alisema Lali
Eneo
la Loliondo limekuwa likikumbwa na vurugu za kikabila mara kwa mara
baina ya wasonjo na wamasai ambapo watu zaidi ya ishirini
wamekwisha poteza maisha katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.kwa upande wao wasonjo wandai kuwa serikali imekuwa ikiwapendelea Wamasai na kuwapa haki zaidi katika mizozoz inayotokea katika eneo hilo yakihusisha ugomvi wa mipaka ya maeneo ya malisho na mifugo baina jamii hizo
indaiwa kuwa wananchi wengi wa jamii hizo wanamiliki silaha za moto ambazo zinaelezwa kuingizwa na Wasomali katika miaka ya hivi karibuni kabala ya kuondoshwa na jeshi la wananchi wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment