Rais
wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kesho anatarajiwa
kuzindua hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha vijijini Wilayani Arumeru
Mkoani Arusha.
Hospitali hiyo ya Olturumet iliyopo katika kata ya Olturumet inatarajiwa kutoa huduma kwa wakazi zaidi ya laki tatu wa halmashauri hiyo ambayo
haikuwa na hospitali baada ya kuundwa kwa halamashauri ya Meru ambayo ilichukua
hospitali ya Wilaya iliyokuwaepo ya West Meru.
Akizungumza na Blog hii Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo Halifa Ida alisema kuwa
hospitali hiyo pia itahudumia wananchi wa kata na vijiji vya jirani kutoka Wilaya ya Longido itakuwa na vitanda vya
kualza wagonjwa 115.
Alisema kuwa hospitali
hiyo imejengwa na serikali kupitia
miradi yake ikiwemo mradi wa maendeleo ya afya ya msingi ,mradi wa maendeleo ya
jamii (TASAF) nguvu za wananchi na wahisani kutoka nchi za ujerumani na
Marekani.
“Hawa wadau wa nje ambao ni Shirika la umoja wa madaktari wa
ujerumani walitusaidia kujenga wadi ya upasuaji, na wodi nyingineya wanaume hakika
wametusogeza kufikia hapa tulipofika”alisema Hida.
Hida alieleza kuwa
hadi kufikia hatua ya kuzinduliwa ujenzi wa wadi ,maabara ,vyumba vya upasuaji
na vipimo mbalimbali gharama zake zinafikia zaidi ya shilingi milioni mia sita.
Alileza kuwa hopitali hiyo itasaidia kutoa huduma ya mama na mtoto
hasa wanawake wajawazito wa Wilaya hiyo ambao wanakatishwa maisha yao kutokana na kujifungulia majumbani kufuatia uhaba wa huduma za afya.
’Ni jambo la faraja sana kwa watu wa jamii za
kifugaji kusogezewa huduma za uhakika za afya ,hospitali hii itachochea ustawi
wa maisha ya jamii hii”alisema Hida.
Rais Kikwete pia anatarajiwa kuzindua Halmashauri
ya Jiji rasmi baada ya mji wa Arusha kupewa hadhi hiyo kisheria mwezi Agosti
mwaka huu,kuzindua chuo kikuu cha Nelson Mandela na baadaye kuhutubia wananchi wa Jiji la
Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini humo.
0 comments:
Post a Comment