VIONGOZI wa Serikali za
wanafunzi wa Vyuo vikuu Kanda ya Kaskazini ,wamelalamikia Bodi ya mikopo wakidai inawanyima mikopo watoto wanaotoka katika
familia zenye maisha duni .
Viongozi
hao walitoa madai hayo katika mkutano wao uliofanyika katika chuo Chuo cha Maendeleo ya jamii Tengeru (CDTI)
uliokuwa na lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi wa
vyuo vikuu nchini.
Akitoa
tamko hilo kamishna wa vyuo vikuu katika serikali za wanafunzi wa kanda hiyo na
Katibu wa Maadili na Utamaduni katika serikali za wanafunzi za nchi
za Afrika Mashariki ,Benard Adam alisema
kuwa ,Serikali haina budi kuchukua hatua za haraka kunusuru watoto
wa maskini.
Alisema kuwa Bodi ya Mikopo haiwatendei haki watoto
kutoka familia duni ,na kudai kuwa wapo wanafunzi ambao wanapatiwa mikopo
ambao wazazai wao wa uwezo mkubwa kiuchumi.
Alisema
kuwa hali ya maisha ya wanafunzi katika vyuo vikuu vingi
inasikitisha hususani kwa wanafunzi wa Kike ambao ,baada ya hali ngumu ya
maisha wamejikuta wakijiingiza katika vitendo vya ngono ,ili waweze kupata ada
na chakula .
Adamu
alisema kuwa ,baadhi ya Viongozi wa Mikopo wamejisahau na kudai
kuwa baadhi ya wanafunzi wananyimwa mikopo kwa madai kuwa hawana kumbukumbu za
mwanafunzi ,wakati akiwa yuko mwaka wa tatu.
Kimsingi
alisema kuwa ni jambo la aibu kwa Bodi hiyo kuwa haina kumbukumbu za mikopo ya
mwanafunzi ambaye imekuwa inampatia mkopo kwa zaidi ya miaka miwili.
Kwa
upande wake Makamu wa Rais Chuo Kikuu Tumaini Makumira ,Sophia Mmbuji
alisema kuwa wanafunzi katika vyuo vikuu wanapata shida ya malazi hususani
wanaoishi nje ya vyuo ,kwa kuwa wanapangisha vyumba kwa kati ya Tshs.70,000
hadi 100,000 wengi wakiwa hawana mikopo .
Mmbuji
alisema kuwa wakati umefika wa Serikali na wadau wa Elimu kuvalia Njuga tatizo
hilo ikiwa ni kuwezesha wanafunzi hao kupangisha pango kwa bei nafuu ,iweze
kulingana na Hosteli za vyuo .
Huwezi
kuamini ,wenye nyumba sasa ,wametugeuza kuwa ni mtaji ,wanaamini tuna
fedha nyingi kwa kuwa tunapatiwa mkopo ,na kufikia hatua kupanga bei ya mapango
ya wanafunzi kuwa ya juu na watu wa kawaida kuwa chini,tunaomba Serikali
ituonee huruma tunaonewa na wenye nyumba ,ifanye mazungumzo nao ,ili kuweza
kukabiliana na hali hii.
0 comments:
Post a Comment