Friday, January 3, 2014


WATU wawili wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi katika machimbo ya kokoto katika eneo la Terat nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Kufuatia tukio hilo  serikali mkoani Arusha imepiga marufuku uchimbaji wa kokoto katika eneo hilo na kuagiza kamati iliyoundwa mwaka jana baada ya ajali kama hiyo kutokea katika eneo la Moshono  kufanya uchunguzi katika migodi yote.

Kwa mujibu wa Mulongo kamati hiyo itatakiwa kuleta mapendekezo  na kuleta mapendekezo ya namna ya  kuboresha hali ya usalama katika machimbo.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa  Mulongo ametoa amri hiyo baada ya kufika katika eneo la tukio na kuongea na viongozi wa eneo hilo.

“Ile kamati sasa itaanza upya kuchunguza hali ya usalama na kuleta mapendekezo  ya kuhakiki hali ya usalama”alisema Mulongo.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Arusha Liberatus Sabas aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Joseph Solomon  (18)na Saimon Petro(15) wote wakazi wa Muriet.

 Katika hatua nyingine jeshi   la polisi Mkoani  Arusha kupitia kwa kamanda Liberatus Sabas limewataka watu wanaomiliki migodi ya uchumbaji wa kokoto kuhakikisha kuwa wana vibali vya kufanya kazi hiyo.

“Tunapiga marufuku haya machimbo yanayoanzishwa kiholela na kuhatarisha maisha ya watu ,tutaanza kufuatilia na kuchukua hatua kwa kushirikiana na vyombo vingine vya serikali”alisema Sabas.
Aliongeza kuwa pia katika migogodi hiyo wahakikishe kuwa kuna usalama wa kutosha ikiwemo miundo mbinu ya tahadhari  na uokoaji.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa lilitokea saa tatu asubuhi leo katika machimbo hayo baada  ngema kuwaangukia vijana waliokuwa wakichimba na kupakia moram katika gari lililofika katika machimbo hayo.
“lilitokea ghafla sana mimi nilikuwa juu mara nikasiakia ngema inakatika yaani nilishuhudia wenzangu wakifunikwa na udongo na kupoteza maisha”alisema manusura Loiruk Sandamu.
Tukio hilo ni la pili kutokea katika machimbo ya kokoto Jijijni Arusha baada ya mwaka  Machi 16 mwaka jana  kuanguka na kufukia watu 16 katika eneo la Moshono.


Wednesday, January 1, 2014

WADAU,wa uhifadhi wanyama pori   kati ya Tanzania na Kenya wameanzisha ushirikiano  wa kudhibiti  ujangili wa wanyama pori  katika  mpaka wa kaskazini  mwa Tanzania




Ushirikiano huo unahusisha kubadilishana taarifa za kihalifu,intelijensia na   kufanya doria za pamoja katika mapito ya wanyama pori  eneo hilo ambalo linaunganisha hifadhi za Arusha ,Kilimanjaro  na hifadhi ya Amboseli ya nchini Kenya

Wakizungumza katika  mkutano wa pamoja uliofanyika  katika eneo la hifadhi  jamii ya wanyama (WMA)  la Enduimet Wilayani Longido, walisema kuwa uwindaji wa tembo na simba katika eneo la mpaka limekuwa ni tatizo kubwa.

Mkuu wa usalama katika eneo la hifadhi jamii la enduimet Imanuel Bujiku alisema kuwa wawindaji wamekuwa wakiwinda wanyama na kukimbilia nchi jirani kukimbia kukamatwa.
Bujiku alisema kuwa  ushirikiano huo umehusisha idara zote za ulinzi usalama  katika nchi zote zikiwemo polisi na vikosi vya kudhibiti ujangili.
“  Lengo  kuu  la ushirikiano  wetu ni wa kuhakikisha eneo  la mapito ya wanyama kutoka hifadhi ya Amboseli Kenya  kuja Tanzania tunaweka ulinzi wa kutosha kuzuia mauaji ya wanyama   “alisema Bujiku
Kuhusu hali ya ujangili katika eneo la Enduimet alieleza kuwa kuanzia  mwezi januari hadi mwezi octoba mwaka huu jumla ya majangili 16  walikamatwa  pamoja  na gari 1  baiskeli 8 pikipiki 5 na watuhumiwa kufikishwa mahakakani
Naye mhifadhi jamii kutoka hifadhi ya Amboseli Kenya Francis Irungu alisema kuwa ushirikiano huo utadhoibiti ujangili na kuleta tija kubwa  katka uhifadhi wanyama pori.
“Hii ndio mbinu sahihi na endelevu ya kulinda wanyama katika nyakati kama hizi zenye changamoto kubwa za kihalifu dhiti ya wanyama pori,”alisema Irungu.
Kwa upande wake Samwel Ole Kaangi kutoka mfuko wa uhifadhi wa  Big  life nchini Kenya alisema kuwa ushirikiano huo umewafanya kuweka mpango kazi na utekelezaji kutokomeza ujangili katika eneo hilo.
“Wanyama wanauawa sana katika eneo hili ,tumekubaliana pamoja na uwezo tunao tutadhibiti ujangili wa tembo na wanyama wengine katika eneo hili”alisema Ole Kaangi.

Time Management

Translator

Popular Posts

Fellow Bloggers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews