Monday, June 17, 2013



WAFUGAJI Mkoani Arusha wametaka serikali na wadau wa maendeleo  kuelimisha viongozi wa serikali za vijiji juu ya sheria ya ardhi na matumizi bora ya ardhi.
Wanadai kuwa ufahamu wa sheria hasa ya ardhi ya vijiji ya mwaka 1999  itasaidia  kuondoa migogoro ya ardhi kati ya wafugaji ,wakulima na wawekezaji.
Wafugaji  hao walisema  ufahamu mdogo wa   viongozi wa serikali za vijiji  juu ya sheria ya ardhi  umesababisha kushindwa kutengeneza matumizi bora ya ardhi na kusababisha kuwepo kwa mgogoro mingi katika jamii.
Mwenyekiti wa kijiji cha Losirwa Wilayani Monduli  George Lukas alisema kuwa vijiji vingi havijatenga maeneo kulingana na makundi mbalimbali zikiwemo sehemu za malisho na za kilimo.
 “Ni lazima viongozi wa serikali za vijiji waelimishwe kutenga maeneo kulingana na na mahitaji yaliyopo na kuhakikisha kuwa wanasimamia sheria ya ardhi”alisema Lukas.
Wafugaji hao walitoa msimamo huo katika mafunzo sheria ya ardhi ya mwaka 1999 yaliyoendeshwa na  Shirika la MPDO Lareto kwa ufadhili wa The Fondation for civil  Society na kufanyika katika vijiji tisa vya wilaya hiyo.
Akizungumzia mafunzo hayo diwani wa viti maalumu kutoka kata ya Selela Napir Engidong alisema kuwa viongozi wa vijiji wameweza kufahamu umuhimu wa kutunza ardhi kwa kupanda miti na kuacha ukataji miti hovyo.
“Upo umuhimu mkubwa wa kushirikisha jamii katika kufanya maamuzi yanayohusu matumizi ya ardhi, Kama wananchi watashirikishwa, migogoro mingi iliyopo vijiji itapungua”alisema  Nengidong.
Naye Mkurugenzi wa MPDO Baraka Laizer alisema kuwa waliendesha mafunzo hayo ili kuondoa migogoro ambayo imekuwa ikisababaisha kukosekana kwa amani katika vijiji.
“Tumeshuhudia watu wakipoteza maisha ,mali kuharibiwa kutokana na migogoro ya ardhi ,tumegundua kuwa njia pekee ya kuleta suluhu ni kwa viongozi na wadau mbalimbali katika vijiji kuelimishwa kuhusu sheria ardhi ya vijiji”alisema Baraka.
Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo Amani Ole Sekino alisema kuwa viongozi wa serikali za vijiji wameeelimshwa kuhusu sheria ya ardhi pamoja na utatuzi wa migogoro kwa kuzingatia sheria.
Alisema kuwa washiriki walifundishwa juu ya umilikaji wa ardhi ,umuhimu wa kuanisha mipaka na kupata hati miliki ya ardhi ili kuilinda ardhi.
MWISHO……

Sunday, June 16, 2013




WATU wawili  wameripotiwa kupoteza maisha na
wengine zaidi ya hamsini kujeruhiwa  katika tukio la mlipuko wa kitu kinachodhaniwa kuwa bomu la kutengenezwa kwa mkono katika mkutano  wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi mdogo wa kata nne za jiji la Arusha  unaofanyika leo.
Tukio hilo limetokea  majira ya saa 12 kasoro katika kata ya  kaloleni kwenye uwanja wa michezo wa Soweto Jijini hapa
Hata hivyo taarifa za hivyo hivyo havijathibitishwa na vyombo vya usalama Mkoani Arusha hadi kufiklia alfajiri ya leo na kutokana na hali ya tharuki iliyokumba Jijij la Arusha jana jioni baada ya tukio hilo kutokea katika mkutano huo am,bao ulihutubiwa na mwenyekiti  wa Chadema Taifa  Freeman Mbowe.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo inaelezwa kuwa mlipuko ulitokea karibu na gari la matangazo wakati makada wa cha,ma hicho wakikusanya sadaka zilizodaiwa kuwa zingesaidia mawakala wa chama hicho katika zoezi la kulinda masilahi ya chama hicho katika uchaguzi huo.
Waandishi wa habari walishuhudia idadi kubwa ya majeruhi wakitibiwa katika hospitali za Seliani na Mount Meru wengi wakiwa na majeraha miguuni ,usoni na mikononi.
Kamanda wa Jeshi la polisi           Mkoani Arusha Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kukataa kusema lolote na kuahidi kutoa taarifa kamili za tukio hilo leo mchana.
Tukio hili ni la pili kutokea katika kipindi kisichozidi miezi miwili baada ya shambulizi la aina hiyo kufanyika katika kanisa la Katoliki parokia Olasiti nje kidogo ya Jijiji la Arusha na kusababisha vifo kadhaa namajeruhi.

Time Management

Translator

Popular Posts

Fellow Bloggers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews