WADAU,wa uhifadhi wanyama pori kati ya Tanzania na Kenya wameanzisha ushirikiano wa kudhibiti ujangili wa wanyama pori katika mpaka wa kaskazini mwa Tanzania
Ushirikiano huo unahusisha kubadilishana taarifa za kihalifu,intelijensia na kufanya doria za pamoja katika mapito ya wanyama pori eneo hilo ambalo linaunganisha hifadhi za Arusha ,Kilimanjaro na hifadhi ya Amboseli ya nchini Kenya
Wakizungumza katika mkutano wa pamoja uliofanyika katika eneo la hifadhi jamii ya wanyama (WMA) la Enduimet Wilayani Longido, walisema kuwa uwindaji wa tembo na simba katika eneo la mpaka limekuwa ni tatizo kubwa.
Mkuu wa usalama katika eneo la hifadhi jamii la enduimet Imanuel Bujiku alisema kuwa wawindaji wamekuwa wakiwinda wanyama na kukimbilia nchi jirani kukimbia kukamatwa.
Bujiku alisema kuwa ushirikiano huo umehusisha idara zote za ulinzi usalama katika nchi zote zikiwemo polisi na vikosi vya kudhibiti ujangili.
“ Lengo kuu la ushirikiano wetu ni wa kuhakikisha eneo la mapito ya wanyama kutoka hifadhi ya Amboseli Kenya kuja Tanzania tunaweka ulinzi wa kutosha kuzuia mauaji ya wanyama “alisema Bujiku
Kuhusu hali ya ujangili katika eneo la Enduimet alieleza kuwa kuanzia mwezi januari hadi mwezi octoba mwaka huu jumla ya majangili 16 walikamatwa pamoja na gari 1 baiskeli 8 pikipiki 5 na watuhumiwa kufikishwa mahakakani
Naye mhifadhi jamii kutoka hifadhi ya Amboseli Kenya Francis Irungu alisema kuwa ushirikiano huo utadhoibiti ujangili na kuleta tija kubwa katka uhifadhi wanyama pori.
“Hii ndio mbinu sahihi na endelevu ya kulinda wanyama katika nyakati kama hizi zenye changamoto kubwa za kihalifu dhiti ya wanyama pori,”alisema Irungu.
Kwa upande wake Samwel Ole Kaangi kutoka mfuko wa uhifadhi wa Big life nchini Kenya alisema kuwa ushirikiano huo umewafanya kuweka mpango kazi na utekelezaji kutokomeza ujangili katika eneo hilo.
“Wanyama wanauawa sana katika eneo hili ,tumekubaliana pamoja na uwezo tunao tutadhibiti ujangili wa tembo na wanyama wengine katika eneo hili”alisema Ole Kaangi.
0 comments:
Post a Comment