WATU
wawili wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi katika machimbo ya kokoto
katika eneo la Terat nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Kufuatia tukio hilo serikali mkoani Arusha imepiga marufuku
uchimbaji wa kokoto katika eneo hilo na kuagiza kamati iliyoundwa mwaka jana
baada ya ajali kama hiyo kutokea katika eneo la Moshono kufanya uchunguzi katika migodi yote.
Kwa mujibu wa Mulongo kamati hiyo itatakiwa kuleta
mapendekezo na kuleta mapendekezo ya
namna ya kuboresha hali ya usalama
katika machimbo.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo ametoa amri hiyo baada ya kufika
katika eneo la tukio na kuongea na viongozi wa eneo hilo.
“Ile kamati sasa itaanza upya kuchunguza hali ya usalama na
kuleta mapendekezo ya kuhakiki hali ya
usalama”alisema Mulongo.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kamanda wa Jeshi la
polisi Mkoani Arusha Liberatus Sabas aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni
Joseph Solomon (18)na Saimon Petro(15)
wote wakazi wa Muriet.
Katika hatua nyingine
jeshi la polisi Mkoani Arusha kupitia kwa kamanda Liberatus Sabas
limewataka watu wanaomiliki migodi ya uchumbaji wa kokoto kuhakikisha kuwa wana
vibali vya kufanya kazi hiyo.
“Tunapiga marufuku haya machimbo yanayoanzishwa kiholela na
kuhatarisha maisha ya watu ,tutaanza kufuatilia na kuchukua hatua kwa
kushirikiana na vyombo vingine vya serikali”alisema Sabas.
Aliongeza kuwa pia katika migogodi hiyo wahakikishe kuwa
kuna usalama wa kutosha ikiwemo miundo mbinu ya tahadhari na uokoaji.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa lilitokea saa tatu
asubuhi leo katika machimbo hayo baada
ngema kuwaangukia vijana waliokuwa wakichimba na kupakia moram katika
gari lililofika katika machimbo hayo.
“lilitokea ghafla sana mimi nilikuwa juu mara nikasiakia
ngema inakatika yaani nilishuhudia wenzangu wakifunikwa na udongo na kupoteza
maisha”alisema manusura Loiruk Sandamu.
Tukio hilo ni la pili kutokea katika machimbo ya kokoto
Jijijni Arusha baada ya mwaka Machi 16
mwaka jana kuanguka na kufukia watu 16
katika eneo la Moshono.
0 comments:
Post a Comment