Friday, November 16, 2012




Wanajeshi wa waasi Congo
Wanajeshi wa waasi Congo

Takriban wapiganaji 150 wa waasi wameuawa kwenye mapigano kati ya wanajeshi wa serikali Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mapigano hayo yanasemekana kuwa mabaya zaidi tangu mwezi Julai wakati waasi wa M23 walipotishia kuuteka mji mkuu wa eneo hilo Goma.
Msemaji wa serikali ya nchi hiyo Lambert Mende amesema waasi 51 waliouawa walikuwa wamevalia sare rasmi ya jeshi la Rwanda.
Serikali ta Rwanda imekanusha madai kuwa inawaunga mkono waasi hao wanaopigania katika eneo hilo lenya utajiri mkubwa wa madini Mashariki mwa Congo.

Hata hivyo hakuna thibitisho rasmi kuhusu idadi ya watu waliouawa na upande wa waasi haujatoa taarifa yoyote kuhusiana na idadi ya wapiganaji wake waliouawa.

Zaidi ya raia laki tano wametoroka makwao tangu Aprili wakati wanajeshi kadhaa walipoasi kutoka jeshini.

Mapigano hayo yamekuwa yakiendelea karibu na kijiji cha Kibumba takriban kilomita 30 Kaskazini mwa Goma.
Gavana wa Jimbo la Kivu ya Kaskazini Julien Paluku ameiambia BBC kuwa mapigano hayo yanaendelea hadi leo siku ya Ijumaa.
Umoja wa Mataifa unazishtumu Rwanda na Uganda kwa kuwaunga mkono waasi, shutuma ambazo zinapingwa na nchi zote mbili.
Mwandishi wa BBC, Gabriel Gatehouse amesema kuzunguka kijiji cha Kibumba kiasi cha kilomita 30 Kaskazini mwa Goma hali imekuwa mbaya zaidi tangu mwezi Julai.
Amesema serikali imepeleka vikosi zaidi, katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na helikopta za kijeshi, pia askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wameonekana katika maeneo ya kijiji cha Kibumba.
Pande zote mbili wamelaumiana kwa kuanzisha mapigano hayo yaliyoanza mapema asubuhi Alhamisi.

Mwandishi wa BBC amesema wakati alipokuwa katika eneo linalodhibitiwa na waasi Jumatano, aliwaona waasi wa M23 ambao pia hujulikana kama Jeshi la Ukombozi la Congo wakisambaza askari wake na kujiandaa kwa vita.

Watu wanakimbilia kuelekea Kusini ambako majeshi ya serikali yanadhibiti maeneo hayo wakiwa wamebeba mizigo yao vichwani.

Baadhi yao wamekuwa wakienda katika kambi kubwa ya Kibai iliyopo katika vitongoji vya kaskazini mwa Goma.

Msema wa Umoja wa Mataifanchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Luteni Kanali Prosper Basse, amesema pia kumekuwa na mapigano kilomita 90 kaskazini mwa Goma, huku majeshi ya serikali yakitwaa mji wa Mabenga na kusonga mbele kuelekea mji wa Kiwanja ambao ni mji muhimu wa waasi.

0 comments:

Post a Comment

Time Management

Translator

Popular Posts

Blog Archive

Fellow Bloggers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews