Thursday, November 15, 2012


Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema hakuna mgonjwa yoyote mpaka sasa  aliyegundulika kuingia nchini akiwa na dalili za ugonjwa mpya wa ‘Marburg’ ulioripotiwa kugundulika kutokea nchini Uganda.

Afisa Habari wa Wizara hiyo, Nsachris Mwamwaja, alisema hayo alipozungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa wizara imechukua tahadhari ya kutosha dhidi ya ugonjwa huo.


Kutokana na hali hiyo, Mwamaja aliwataka wananchi kutokuwa na wasiwasi kwani wizara imejipanga kikamilifu kuhakikisha ugonjwa huo, ambao hauna tiba wala chanjo, hauingii nchini.


Hata hivyo, aliwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.


Oktoba 25, mwaka huu, wizara hiyo ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikieleza kupokea taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) ikielezea kuripotiwa kuzuka kwa ugonjwa huo nchini humo.


Maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huo yalitajwa kuwa ni Wilaya ya Kabale, iliyoko Kanda ya Kusini Magharibi mwa Uganda.


Wilaya hiyo inapakana na nchi ya Rwanda na mpaka Oktoba 24, mwaka huu, watu 13 waliripotiwa kuambukizwa na wengine sita kupoteza maisha.

 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

Time Management

Translator

Popular Posts

Blog Archive

Fellow Bloggers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews