Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kutotumia
muda mwingi kuvishambulia vyama vya siasa.
Badala yake Dk. Slaa amemtaka Rais Kikwete
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutumia muda huo
kuzungumza jinsi ya kutatua kero za wananchi ili kupunguza ukali na
ugumu wa maisha unaowakabili sasa.
Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari katika Mahakama Kuu ya Kanda ya Arusha kuhusiana
hoja mbalimbali zilizozungumzwa katika mkutano wa CCM uliofanyika jijini
Dar es Salaam juzi.
Akijibu shutuma mbalimbali zilizotolewa
katika mkutano wa kuwapokea viongozi mbalimbali wa CCM waliochaguliwa
mjini Dodoma, Dk. Slaa alisema katika mkutano huo viongozi wengi wa
chama hicho akiwamo Rais Kikwete, walitumia muda mwingi kuelekeza nguvu
zao jinsi ya kukabiliana na vyama pinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka
2015.
Alisema CCM imeelekeza nguvu zake kujifua
ili kukikabili Chadema katika uchaguzi ujao na siyo kuwaeleza wananchi
nini watawafanyia ili kuwaondoa katika janga la umaskini.
Aidha, aliwatuhumu viongozi wa CCM
kuchukua sera mbalimbali zilizoanzishwa na Chadema ikiwamo ya kusomesha
wanafunzi bure kutoka shule ya msingi hadi sekondari.
Aidha, alisema anashangaa uteuzi wa Katibu Mkuu wa ccm, Abdulrahman Kinana kwa madai kwamba siyo msafi.
0 comments:
Post a Comment