MBUNGE wa Jimbo la Arumeru
Mashariki kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Joshua
Nasari amesusia kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri
ya Meru ,baada ya kamati ya Uchumi ,Ujenzi na Mazingira ,kutaka kupitisha
azimio la kugawa viwanja eneo la Soko la Tengeru.
Mbunge huyo alidai kuwa alichukua
uamuzi huo baada ya kuona baraza hilo
kukiuka makubaliano ya awali ya kujenga vitega uchumi katika eneo hilo na kudai
kuwa anahisi kuna mchezo wa kifisadi unaotaka
kufanywa.
“Awali tulikubvaliana kujenga vitega
uchumi leo wabadilisha kinyemela wanataka kutengeneza mlango wa kufanya ufisadi
siwezi kushiriki kubariki jambo hilo kamwe”alisema Nassari akizungumza na waandishi
wa habari.
Alisema kuwa ana historia ndefu iayoonyesha kuwa siku zote Viwanja vikitolewa wanaokuja kununua ni watu
wa Arusha mjini ,watu wa Moshi na watu wa Meru hawaambulii chochote.
Alisema kuwa kwa maoni yake ni faida zaidi kujenga vitega
uchumi ili wananchi waje wafanyie
biashara badala ya kugawa kama Kamati ya Uchumi ilivyopendekeza.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la
Madiwani Frida Kaaya akielezea sakata hilo aliliambia Baraza hilo kuwa
ameshangazwa na maamuzi ya Mbunge huyo ambaye alisema ni Diwani akiwa katika
Baraza hilona alipaswa kukubali maamuzi
ya Madiwani wenzake .
Alisema kuwa viwanja vinavyotarajiwa
kugawanywa ni Viwanja 118 ,vitakavyojengwa kuzunguka soko na hivyo kufanikiwa
kuwaondoa wafanyabiashara wanaopanga bidhaa chini .
Alifafanua kuwa kwa sasa Halmashauri
hiyo imeanza kujikita kusaidia Vijana ,na kuwa kugawanywa viwanja hivyo
kutalenga vikundi vya vijana ,ili waweze kufungua miradi ya maendeleo
kupitia vikundi,hatimaye kuweza kujikwamua katika uchumi na kuongeza kipato
chao .
Diwani wa Kata ya Nkwarusambo
akizungumza katika kikao hicho alimtaka Diwani Nassari kuheshimu maamuzi ya
vikao vya baraza na kushirikiana na madiwani wenzake kulewatea wananchi
maendeleo na siyo kupinga kila kitu hata kama ni jambo jema .
Alisema kuwa Halmashauri hiyo
,inasifiwa kuwa na ushirikiano mzuri na wananchi ,na kuwa Mbunge huyo anatakiwa
kuepuka migogoro isiyokuwa na na lazima .
0 comments:
Post a Comment