Friday, November 23, 2012


WATU zaidi ya mia moja katika kijiji Cha Ngabobo Wilayani Arumeru  Mkoani Arusha  hawana mahala pa kuishi baada ya nyumba zao kubomolewa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali katika eneo hilo.

Wakizungumza na waandishi wa habari wananchi hao walisema kuwa mvua hizo zilinyesha kwa muda wa nusu saa na kuangusha mamia ya miti ,kubomoa na kuharibu barabara na kusababisha mawasiliano katika eneo hilo kuwa magumu.

Mwenyekiti wa kijiji  hicho Zabulon Kimaki alisema kuwa tukio la limeacha  kaya zaidi ya  ishirini zenye watu mia  moja na  thelathini  zikiwa  hazina mahali pa kuishi.

 “Hali ilikuwa ya kushutua sana ,mvua hiyo ilikuwa sio ya kawaida lakini kibaya limesababisha watu takariban mia moja na ishirini kulala nje kutoakana na mabati ya nyumba zao kuezuliwa na upepo,hawajaweza hata kuokoa kpande cha bati na hatujui yalipo mapaa na bati zilizoezuliwa na upepo”alisema Kimaki.
Alisema kuwa watoto zaidi ya themanini wameshindwa kwenda shule kufuatia tukio hilo kusababisha kupoteza ama kuharibiwa vifaa vya shule kama vile  madaftari ,vitabu na sare za shule kusombwa na maji.

Alisema serikali inapaswa kuwapelekea huduma za kijamii wananchi hao ikiwemo mahema na chakula ili kuweza kuwasaidia kukabili hali waliyo nayo kwa sasa.

“Uongozi wa halmashauri ulifika jana hapa kungalia madhara yaliyotokea lakini hawajatoa chochote ila tunamshukuru Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari kwa kutoa chakula ambacho kitawasaidia  wahanga hawa  kujikimu kwa siku chache”alisema Kimaki.

Mmoja wa wahanga wa tukio hilo Sambeke Saiteru alisema kuwa kwa sasa wanalala nje pamoja na familia yake hali ambayo imefanya watoto wake kuanza kuumwa kifua kuitokana na baridi kali nyakati za usiku.

Alieleza kuwa licha ya upepo kuezua paa la nyumba yake lakini pia maji yaliyotririka kwa wingi yaliingia ndani na kusomba vyakula na vyombo vya nyumbani na sasa kubaki bila chochote.
“Hapa nilipo nimebaki na nguo nilizovaa toka siku ya tukio ,hata watoto wangu saba nao hawana mavazi maji ya mvua ilisomba kila kitu hapa nyumbani,tungefurahi kupata msaada wa haraka kutoka serikalini”alisema Saiteru. 

Alisema kuwa tukio hilo limeacha hofu katika familia yake kwani lilitokea wakiwa ndani ya nyumba yao .
Mwananchi mwingine  Edward Ngoiyo alisema tukio hilo pia lilitokea akiwa na familia yake ndani ya nyumba ambapo alisema alishangaa kuona paa lote likipigwa na upepo na kuondolewa na kuchwa wakinyeshewa.
“Watoto wangu walichanganganyikiwa ,hali ilikuwa ni ya kutisha ,tumepoteza nguo vitabu vya watoto na wa kwangu wawili  wameshindwa kwenda shule kutokana na janga hili”alisema Ngoiyo.
Alisema kuwa kwa sasa anaishi na familia yake katika zizi la ngombe hali ambayo inaendelea kuhatarisha maisha yake  na familia aliyo nayo.

Alisema kuwa halmshauri walifika na Mbunge na kutoa msaada wa  chakula  kwa waathirika kwa kila mmoja kupata kilo mbili za mchele na sukari kilo moja.

“Tunaomba wafanye haraka kutuokoa katika hali hii ,hatukutarajia imetokea kwa kasi na ghafla na kufanya halii hii tuliyo nayo”alisema Ngoiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru  Nyirembe  Munasa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tayari uongozi wa halimashauri ya Meru umekwishafika katika eneo la tukio kufanya tathmini ya madhra yaliyotokea.

“Ni kweli tukio limetokea ila mimi niko safarini ila nimekwisha  agiza uongozi wa halmashauri  kwenda katika eneo la tukio kufanya tathmini na kutoa msaada unaohitajika lakini pia Mbunge Joshua Nassari alifika na kutoa msaada wa chakula ”alisema Munasa.

Alisema katika timu hiyo ya halimashauri wapo watu wanaohusikama masuala ya maafa na wahandisi wa ujenzi wa halaimashauri hiyo.
MWISHO…

0 comments:

Post a Comment

Time Management

Translator

Popular Posts

Blog Archive

Fellow Bloggers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews