WATU sita wamefariki dunia popo hapo katika ajali mbaya
iliyotokea katika barabara ya Arusha Namanga eneo la Longido Mkoani Arusha
likihusisha gari dogo la abiria na lori la mizigo.
Gari la abiria lililoua watu sita |
Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Jeshi la polisi Mkoani
Arusha lilitokea 5 za usiku wa kuamkia
jana na kusabaisha abiria sita waliokuwa katika gari dogo aina ya noa kupoteza
maisha baada ya gari dogo aina ya Noah kugongana uso kwa uso la lori la mizigo.
Mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa gari dogo ambalo
lilikuwa likitokea Arusha likiwabeba wapishi waliokuwa wakitokea jijini Arusha
kwenda Longido kwa ajili ya sherehe za kipaimara na harambee ya kumalizia ujenzi wa kanisa la KKKT.
Harambee hiyo ilikuwa iongozwe na waziri Mkuu mstaafu Edward
Lowasa na katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.
“Nilikuwa wa kwanza kufika katika eneo la ajali nilishiriki
kutoa miili sita ya watu waliopotea maisha wengine wawili walikuwa na hali
mbaya wapo Hospitali “alisema Sendeu Parmwat shuhuda na mkazI wa Longido.
Parmwat alisema kuwa watu wote waliofariki papo ni wapishi
waliokuwa wakiongozwa na mtaalamu wa mapishi anayejulikana kwa jina maarufu la
Bonge Jijini hapa.
Alisema kuwa polisi walifika muda mfupi na kuanza kuchukua
miili ya marehemu pamoja na kuwapeleka majeruhi katika hospitali ya Mkoa wa
Arusha Mount Meru.
Shuhuda mwingine Stephano Laiser alieleza kuwa lori
lililosababaisha maafa hayo lilikuwa limepaki pembeni ya barabara na halikuwa
na taa.
Akizungumzia kuhusu ajali hiyo kamanda wa jeshi la polisi
Mkoani Arusha Liberartus Sabas alisema kuwwatu hao wali[poteza maisha na
wengine wawili wamelazwa hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.
“Abiria sita katika Noa yenye namba T 329AWJ walipoteza maisha na hakuna majeruhi yeyote
katika lori ,tunaendelea na uchunguzi lakini taarifa za awali zinaonyesha kuwa
Noa ilikuwa katika mwendo kasi”alisema Kamanda Sabas.
Aliwataja marehemu waliotambuliwa kuwa ni Hamidu Msala maarufu kwa jina la
Bonge,Habibu waziri ,Faridah Ibrahim ,Martha Gabriel wote wakazi wa Jiji la
Arusha wengine wawili bado hawajatambuliwa.
Waandishi wa habari walishuhudia ndugu jamaa za marehemu wakiwa katika uwanja
wa eneo la kuhifadhi maiti katika hospitali ya Mkoa wa Arusha kufuatilia habari
za ndugu zao.
Naye muuguzi wa zamu katika hospitali ya Mount Meru ambaye
hawakuwa tayari kutaja jina alithibitisha kuwepo kwa majeruhi wawili ambao alisema hali zao ni mbaya.
“Wako katika uangalizi wa juu ,majreha ni makubwa sana mmoja
yuko hoi lakini tunajitahidi kuokoa maisha yao”alisema Muuguzi huyo.
Mwisho……
0 comments:
Post a Comment