Sunday, May 5, 2013


Habari zilizopatikana hivi punde zinaeleza kuwa kumetokea mlipuko wa kitu kinachodhaniwa kuwa bomu katika Parokia mpya ya OLasiti  katika jimbo kuu la Arusha ambayo ilikuwa inazinmduliwa rasmi.

 Inaelezwa na baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo lililotokea saa tano kasoro asubuhi kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa na wamekimbizwa hospitali kupata matibabu.

kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Arusha Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mpaka sasa hakuna mtu aliyepoteza maisha kufuatia tukio hilo.

"Mlipuko umetokea vyombo vya usalama vipo hapa kufanya uchunguzi ,ninachoweza na mtu mmoja amepoteza maisha. 

Alisema kuwa watu 42 wamejerihiwa vibaya na polisi wanamshikilia mtu mmoja ambaye polisi wanasema wanamhoji kuhusu tukio hilo.

Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa bomu hilo lilirushwa na watu waliofika karibu na kanisa hilo wakivalia nguo za kuficha nyuso wakiwa katika gari ambayo namba zake hazikuweza kufamika na kurusha kitu ambacho kililipuka karibu na meza ya misa takatifu.

Misa hiyo ilikuwa inaendeshwa na Balozi  wa Vatican na mjumbe maalum wa Papa nchini Tanzania  Francisco Padila .

hadi kufika saa 8 mchana watu 42 walikuwa  wamejeruhiwa ibaya  katika ibada hiyo.

Mtu mmoja aliyetajwa kuwa ni Regina Loningo Kuresoi amepoteza maisha katika tukio hilo.

Maafisa wa jeshi la polisi ,askari wa jeshi la wananchi kikosi cha mabomu wapo katika eneo la tukio.


1 comment:

Time Management

Translator

Popular Posts

Fellow Bloggers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews