Hatimaye mwili wa askofu wa Kanisa la Kilutheri
Tanzania (KKKT) Dayosisi yaKaskazini Kati,Marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer unatarajiwa
kuzikwa Ijumaa ya wiki ijayo Februari 15, 2013.
Taarifa
iliyotolewa na Kamati ya Mazishi ya KKKT na Familia ya Marehemu, iimeeleza kuwa
Marehemu atazikwa katika eneo la Kanisa Kuu mjini Kati Arusha.
Aidha taarifa
hiyo inasema kuwa waumini na Washirika wa Kanisa Kuu na makanisa yote ya KKKT
nchini, Wananchi, ndugu jamaa na marafiki watapata fursa ya kutoa heshima zao
za mwisho kwa Mwili wa marehemu kuanzia siku
y Alhamisi mchana ya Februari 14, 2013.
Taarifa hiyo
iliongeza kuwa Mwili wa Askofu Laizer utalala Kanisani hapo hadi Ijumaa ya
Mazishi.
Marehemu Askofu
Thomas Laizer aliyezaliwa Machi 10, 1945 katika Kijiji cha Kitumbeine Wilayani Longido na
baade kupata elimu yake ya msingi hadi darasa la nane Longido na kumaliza mwaka
1965.
Askofu Laizer,
aliendelea na masomo yake ya juu ndani na baade kujiunga na masomo ya Theolojia
katika chuo cha Makumira na baade kuongeza masomo nchini Marekani.
Marehemu wakati
wa uhai wake alikuwa Mwinjilisti, Mchungaji katika makinisa mbalimbali nchini
na baade kuwa Mkuu wa Jimbo na Mkuu wa Sinodi na baade kuwa Rais wa sinodi
kabla ya kusimikwa rasmi kuwa Askofu wa Kwanza wa Dayosisi ya Arusha ambayo kwa
sasa ni Dayosisi ya Kaskazini Kati.
0 comments:
Post a Comment