Friday, January 18, 2013

 

Jasusi Denis Alex
Kundi la wanamgambo la kiisilamu Al-Shabab, limesema kuwa limemuua jasusi wa Ufaransa ambaye walikuwa wamemzuilia.
Inaarifiwa Al Shaabab wamemuua Jasusi Denis Alex baada ya jaribio la makomando wa Ufaransa la kumuoka kutibuka.
Serikali ya Ufaransa imesema inaamini kuwa Allex aliuawa wiki jana wakati wa jaribuio la kumuokoa ambapo pia makomando wawili wa ufaransa waliuawa.

Allex alitekwa nyara nchini Somalia mwezi Julai mwaka 2009.
Wanamgambo wa Al-Shabaab, ambao wana uhusiano na al-Qaeda, walisema kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa Allex aliuawa siku ya Jumatano.

Awali Al-Shabab walitishia kumuua Allex na kusema ni kwa sababu ya jaribio la makomando wa Ufaransa kutaka kumuokoa wakisema kuwa Ufaransa inapaswa kulaumiwa kwa kifo chake.
Siku ya Jumatano,takriban makomando hamsini walishambulia kwa helikopta ngome ya al-Shabab katika eneo la Bulo Marer, wakiamini kuwa Allex alikuwa anazuiliwa mjini humo.
Aidha Al-Shabaab walisema kuwa iwalikuwa na habari ya kuwa shambulio lingetoa dhidi yao na kwamba Alex hakuwepo mjini Bulo wakati huo.
Ufaransa inasema kuwa wanamgambo 17 waliuawa wakati wa makabiliano kati yao na makomando wa Ufaransa, na kwamba yalidumu kwa saa moja.  
Raia kadhaa waliuawa wakati wa makabiliano hayo.
Kwa upande ake, Ufaransa inasema kuwa ililazimika kufanya mashambulizi hayo baada ya kushindwa kumuokoa

Serikali ya Somalia ilisema kuwa haikuwa na taarifa zozote kuhusu mashambulizi hatyo na kuwa inasikitishwa sana na vifo vya raia.

Mnamo Jumatatu, al-Shabab ilichapisha picha ya mwanajeshi wa Ufaransa ambaye kundi hilo linasema alifariki kutokana na majeraha ya risasi,wakati wa uvamizi. 

Somalia haijakuwa na serikali thabiti kwa zaidi ya miongo miwili.

Nayo ufaransa ina kambi kubwa ya kijeshi katika nchi jirani ya Djibouti, ikiwemo kikosi cha jeshi la wanamaji na wanahewa.

0 comments:

Post a Comment

Time Management

Translator

Popular Posts

Follow by Email

Fellow Bloggers

Google+ Followers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews