Uhuru Kenyata aameshinda
kiti cha urais kupitia Muungano wa Jubelee katika uchaguzi ulio malizika kwa kura kuhesabiwa na kuhakikiwa katika
makao makuu ya ya kuhesabu kura katika
eneo la Bomas Jijini a Nairobi.
Kufikia saa
8:30 usiku Uhuru alikuwa mbele
kwa kura 6,173,433 dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga aliyekuwa na kura
5, 340,546 ikiwa ni tofauti ya kura 832,887 na majimbo yaliyo kwisha kutangazwa
ni 291/291.
Kwa mujibu wa tume ya
uchaguzi nchini Kenya IEBC jumla ya kura zote zilizopigwa na kuhesabiwa
kwa nafasi ya Urais ni kura 12,338, 667 kutoka katika majimbo yote ya
Uchaguzi 291 huku kura zilizoharibika zikiwa 108975 na kura halali zikibaki
12,222,980.
Katika kinyang’anyiro
hicho Wycliffe Musalia Mudavadi anashika nafasi ya tatu akiwa amejikusanyia
kura 483,981 nafasi ya nne ikienda kwa Peter Kenneth mwenye kura 72,786.
Mgombea wa Alliance
for Real Change,Mohamud Abduba Dida anashika nafasi ya tano akiwa na kura
52,848 akifuatiwa na Mwana mama Martha Karua wa National Rainbow
Coalition mwenye kura 43,881 hadi sasa.
Nafasi ya saba katika
wagombea hao Urais inakwenda kwa James ole Kiyiapi wa Chama cha Restore and
Build Kenya ambaye ana kura 40,998 huku nafasi ya ya nane na mwisho ikishikwa
na Paul Kibugi Muite wa chama cha Safina.
Matokeo hayo yatatangazwa rasmi leo saa saa 5 asubuhi,
0 comments:
Post a Comment