Monday, June 17, 2013WAFUGAJI Mkoani Arusha wametaka serikali na wadau wa maendeleo  kuelimisha viongozi wa serikali za vijiji juu ya sheria ya ardhi na matumizi bora ya ardhi.
Wanadai kuwa ufahamu wa sheria hasa ya ardhi ya vijiji ya mwaka 1999  itasaidia  kuondoa migogoro ya ardhi kati ya wafugaji ,wakulima na wawekezaji.
Wafugaji  hao walisema  ufahamu mdogo wa   viongozi wa serikali za vijiji  juu ya sheria ya ardhi  umesababisha kushindwa kutengeneza matumizi bora ya ardhi na kusababisha kuwepo kwa mgogoro mingi katika jamii.
Mwenyekiti wa kijiji cha Losirwa Wilayani Monduli  George Lukas alisema kuwa vijiji vingi havijatenga maeneo kulingana na makundi mbalimbali zikiwemo sehemu za malisho na za kilimo.
 “Ni lazima viongozi wa serikali za vijiji waelimishwe kutenga maeneo kulingana na na mahitaji yaliyopo na kuhakikisha kuwa wanasimamia sheria ya ardhi”alisema Lukas.
Wafugaji hao walitoa msimamo huo katika mafunzo sheria ya ardhi ya mwaka 1999 yaliyoendeshwa na  Shirika la MPDO Lareto kwa ufadhili wa The Fondation for civil  Society na kufanyika katika vijiji tisa vya wilaya hiyo.
Akizungumzia mafunzo hayo diwani wa viti maalumu kutoka kata ya Selela Napir Engidong alisema kuwa viongozi wa vijiji wameweza kufahamu umuhimu wa kutunza ardhi kwa kupanda miti na kuacha ukataji miti hovyo.
“Upo umuhimu mkubwa wa kushirikisha jamii katika kufanya maamuzi yanayohusu matumizi ya ardhi, Kama wananchi watashirikishwa, migogoro mingi iliyopo vijiji itapungua”alisema  Nengidong.
Naye Mkurugenzi wa MPDO Baraka Laizer alisema kuwa waliendesha mafunzo hayo ili kuondoa migogoro ambayo imekuwa ikisababaisha kukosekana kwa amani katika vijiji.
“Tumeshuhudia watu wakipoteza maisha ,mali kuharibiwa kutokana na migogoro ya ardhi ,tumegundua kuwa njia pekee ya kuleta suluhu ni kwa viongozi na wadau mbalimbali katika vijiji kuelimishwa kuhusu sheria ardhi ya vijiji”alisema Baraka.
Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo Amani Ole Sekino alisema kuwa viongozi wa serikali za vijiji wameeelimshwa kuhusu sheria ya ardhi pamoja na utatuzi wa migogoro kwa kuzingatia sheria.
Alisema kuwa washiriki walifundishwa juu ya umilikaji wa ardhi ,umuhimu wa kuanisha mipaka na kupata hati miliki ya ardhi ili kuilinda ardhi.
MWISHO……

0 comments:

Post a Comment

Time Management

Translator

Popular Posts

Follow by Email

Fellow Bloggers

Google+ Followers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews