Wednesday, October 31, 2012

VIONGOZI wa Serikali za wanafunzi wa Vyuo vikuu Kanda ya Kaskazini ,wamelalamikia  Bodi ya mikopo wakidai inawanyima  mikopo  watoto  wanaotoka katika familia zenye maisha duni  .

Viongozi hao  walitoa madai hayo katika mkutano wao uliofanyika  katika chuo Chuo cha  Maendeleo ya jamii  Tengeru (CDTI) uliokuwa na lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi wa vyuo vikuu nchini.

Akitoa tamko hilo kamishna wa vyuo vikuu katika serikali za wanafunzi wa kanda hiyo na Katibu wa Maadili  na Utamaduni  katika serikali za wanafunzi za nchi za  Afrika Mashariki ,Benard Adam  alisema kuwa ,Serikali haina budi  kuchukua hatua za haraka kunusuru  watoto wa maskini.

 Alisema kuwa  Bodi ya Mikopo  haiwatendei haki watoto kutoka familia duni ,na kudai kuwa wapo wanafunzi ambao wanapatiwa mikopo  ambao wazazai wao  wa uwezo mkubwa kiuchumi.

Alisema  kuwa hali ya maisha ya  wanafunzi  katika vyuo vikuu vingi inasikitisha hususani kwa wanafunzi wa Kike ambao ,baada ya hali ngumu ya maisha wamejikuta wakijiingiza katika vitendo vya ngono ,ili waweze kupata ada na chakula .

Adamu alisema kuwa  ,baadhi ya Viongozi wa Mikopo wamejisahau  na kudai kuwa baadhi ya wanafunzi wananyimwa mikopo kwa madai kuwa hawana kumbukumbu za mwanafunzi ,wakati akiwa yuko mwaka wa tatu.

Kimsingi alisema kuwa ni jambo la aibu kwa Bodi hiyo kuwa haina kumbukumbu za mikopo ya mwanafunzi ambaye imekuwa inampatia mkopo kwa zaidi ya miaka miwili.
Kwa upande wake  Makamu wa Rais Chuo Kikuu Tumaini Makumira ,Sophia Mmbuji alisema kuwa wanafunzi katika vyuo vikuu wanapata shida ya malazi hususani wanaoishi nje ya vyuo ,kwa kuwa wanapangisha vyumba kwa kati ya Tshs.70,000 hadi 100,000 wengi wakiwa hawana mikopo .

Mmbuji alisema kuwa wakati umefika wa Serikali na wadau wa Elimu kuvalia Njuga tatizo hilo ikiwa ni kuwezesha wanafunzi hao kupangisha pango kwa bei nafuu ,iweze kulingana na Hosteli za vyuo .

Huwezi kuamini ,wenye nyumba sasa ,wametugeuza  kuwa ni mtaji ,wanaamini tuna fedha nyingi kwa kuwa tunapatiwa mkopo ,na kufikia hatua kupanga bei ya mapango ya wanafunzi kuwa ya juu na watu wa kawaida kuwa  chini,tunaomba Serikali ituonee huruma tunaonewa na wenye nyumba ,ifanye mazungumzo nao ,ili kuweza kukabiliana na hali hii.

0 comments:

Post a Comment

Time Management

Translator

Popular Posts

Blog Archive

Fellow Bloggers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews