Thursday, October 24, 2013

MTANDAO wa   mashirika ya wafugaji Tanzania (Tanzania Pastoralist Community Forum)umelaani vitendo vya ukatili na ukiukaji wa haki za binadamu ,unaofanywa  katika  operationi tokomeza Majangili inayoendeshwa  na serikali kwa lengo la kutokomeza ujangili dhidi ya wanyama pori

Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari  wadau hao wamedai kuwa zoezi hilo  limejaa matukio ya kusikitisha  na ya kudhalilisha  wananchi pia limesababaisha mamia ya watu kukimbia makazi yao kwa hofu ya kukamatwa.

Mratibu wa mtandao huo  Joseph Ole Parsambei amewaambia waandishi wa habari kuwa operationi hiyo imewatesa watu katika maeneo mbali mbali nchini na kama serikali haitaaangalia ukiukwaji wa sheria watalazimika kuiomba mahakama ilisitishe.

Alisema wafuagaji kutoka katika Wilaya za  Monduli ,Longido ,Simanjiro  na Wilaya ya Chunya  Mkoani Mbeya wamekuwa wahanga wakubwa wa vitendo hivyo.

Alifafanua kuwa  katika wilaya ya Monduli Kata ya Mswakini, watu wanne wamekamatwa na kupelekwa kusikojulikana  hadi sasa  na wengine kukimbia makazi yao  kwa hofu ya kukamatwa .

Wilaya ya Ngorongoro kijiji cha Ololosokwan watu 13 wamekamatwa na mifugo yao zaidi ya 2000 inashikiliwa Wilaya ya Serengeti ikiwa ni baada ya wiki mbili .

Wilaya ya Londido kijiji cha Oromba watu  nane wamekamatwa  kwa sababu hizo ,kupigwa na kunyanyaswa .

Katika Wilaya ya Simanjiro watu wawili wamekamatwa na kupigwa ,nyumba zao  kuchomwa na moto  na Wilaya ya Chunya Ng’ombe 169 zimetaifishwa  na mfugaji mmoja aliyetajwa jina la Magaka Ninya aliuwawa katika zoezi hilo .

Waziri wa mali asili na utalii  Balozi Khamisi Kagasheki alipoulizwa kuhusu madai hayo alikanusha na kusema kuwa zoezi hilo la kusaka mtandao wa ujangili hapa nchini linaendelea vizuri.

0 comments:

Post a Comment

Time Management

Translator

Popular Posts

Follow by Email

Fellow Bloggers

Google+ Followers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews