WATU 872 kutoka kaya 72 katika
kata ya Bwawani Wilayani Areumeru Mkoani Arusha ,hawana mahali pa kuishi
baada ya nyumba zao kusombwa na maji pamoja na samani zao zao za ndani .
Mvua hizo pia zimeharibu mamia ya hekari zenye mazao
mbalimbali zilizokuwa zimepandwa na wananchi wa kata ya
Bwawani katika vijini vya Temi ya Simba na Kijiji cha Bwawani .
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Wilayani
humo ,Fidelist Lumato Mvua hizo zilinyesha mwishoni mwa wiki na kufanya
uharibu mkubwa ,na kuathiri zaidi watu
waliokuwa wakiishi katika maeneo ya mabondeni
Lumato amewataka wananchi wanaoishi wanaoishi katika maeneo ya
mabonde kuhama ikiwa ni kuepusha madhara zaidi yanayoweza kutokea
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha .
Aidha aliwataka kujenga nyumba imara kwa kutumia matofali
yakuchoma ikiwa ni kuepusha madhara ya nyumba zao matope kusombwa na maji
Kufuatia maafa hayo wadau mbali mbali wamejitokeza
kusaidia watu hao ambao ni Halmashauri imetoa msaada wa magunia 180 ya mahindi
kwa ajili ya watu hao ,mbegu za mazo zenye thamani ya million 4.
Wengine waliotoa msaada ni Kampuni ya
Monaban iliyotoa kilo 2000 za unga wa mahindi ,Kampuni ya Tanform
magodoro 50 na unga kilo 200,Red cross msaada wa mablanketi 100,ndoo 50 za
kuchotea maji na Kampuni ya A-Z vyandarua 250 na
Tisheti 200 ,Diwani wa kata ya Mlangarini Mathias Manga ametoa
mabati 100 .
Akitoa ufafanuzi zaidi alisema kuwa hali za watu hao ni ngumu na
kuomba wadau zaidi kujitokeza kuwasaidia waathirika hao .
Lumato alisema hao kwa sasa watu hao wamepatiwa hifadhi katika
ofisi ya kijiji cha bwawani na Kanisani,
Mwisho………………………………………………………………..