Sunday, March 30, 2014

WATU 872  kutoka  kaya 72  katika  kata ya Bwawani Wilayani Areumeru Mkoani Arusha ,hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kusombwa na maji  pamoja na samani zao zao za ndani .

Mvua hizo pia zimeharibu mamia ya hekari zenye mazao mbalimbali   zilizokuwa zimepandwa na wananchi wa kata ya Bwawani katika vijini vya Temi ya Simba na Kijiji cha Bwawani .

Akizungumza na waandishi wa habari  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha  Wilayani  humo ,Fidelist Lumato Mvua hizo zilinyesha mwishoni mwa wiki na kufanya uharibu mkubwa ,na  kuathiri zaidi watu waliokuwa wakiishi katika maeneo ya mabondeni

Lumato amewataka wananchi wanaoishi wanaoishi katika maeneo ya mabonde kuhama ikiwa ni kuepusha madhara zaidi  yanayoweza kutokea kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha .

Aidha aliwataka kujenga nyumba imara kwa kutumia matofali yakuchoma ikiwa ni kuepusha madhara ya nyumba zao matope kusombwa na maji

Kufuatia maafa hayo wadau mbali mbali  wamejitokeza kusaidia watu hao ambao ni Halmashauri imetoa msaada wa magunia 180 ya mahindi kwa ajili ya watu hao ,mbegu za mazo zenye thamani ya million 4.

Wengine  waliotoa msaada ni  Kampuni ya Monaban  iliyotoa kilo 2000 za unga wa mahindi ,Kampuni ya Tanform magodoro 50 na unga kilo 200,Red cross msaada wa mablanketi 100,ndoo 50 za kuchotea maji  na Kampuni ya A-Z vyandarua  250 na Tisheti  200 ,Diwani wa kata ya Mlangarini Mathias Manga ametoa mabati 100 .

Akitoa ufafanuzi zaidi alisema kuwa hali za watu hao ni ngumu na kuomba wadau zaidi kujitokeza kuwasaidia waathirika hao .

Lumato alisema hao kwa sasa watu hao wamepatiwa hifadhi katika ofisi ya kijiji  cha bwawani na Kanisani,

Mwisho………………………………………………………………..


0 comments:

Post a Comment

Time Management

Translator

Popular Posts

Fellow Bloggers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews