Sunday, April 13, 2014

WATU 17  wamejeruhiwa  watano hali zao zikielezwa kuwa mbaya  baada ya kitu kinachodhaniwa  kuwa ni bomu kulipuka katika baa iitwayo night Park katika eneo la Mianzini Jijini Arusha.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kumakia  leo  katika baa hiyo maarufu kwa kuwa na wateja wengi nyakati za jioni.
,
Watu walionusurika  John Bugege  na Lewis Nyali wakizungumza na waandishi wa habari muda mfupi  baada ya mlipuko kutokea walisema kuwa hawakuweza kujua namna tukio lilivyotokea na kwamba walisikia kishindo  kikubwa na watu kuanza kukimbia huku na kule na wengi kujeruhiwa kutokana na kukanyagana.

“Siwezi kueleza hasa nini kimetokea namshukuru Mungu nimetoka salama “alisema alamnusura mwingine Alfred Shayo.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Saba alithibitisha kutoke akwa tukio hilo na kuongeza kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha mlipuko huo na wahusika wa tukio hilo.

“Ni mapema mno kusema chochote majeruhi ni 17 na tayari wapo hospitali ya Mkoa Mount Meru kwa matibabu,,tutawapa taarifa zaidi kesho asubuhi”alisema Sabas katika eneo la tukio.



Tukio hilo ni la tatu kutokea kwa nyakati tofauti  ikiwemo la mlipuko katika kanisa katoliki Olasiti   na la pili katika mkutano wa siasa katika eneo la Soweto  na matukio hayo kusababaisha vifo kadhaa na majeruhi wengi.

1 comment:

  1. Asante kwa taarifa Charles. Arusha panahitajika uchunguzi wa kina

    ReplyDelete

Time Management

Translator

Popular Posts

Fellow Bloggers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews