Tuesday, May 7, 2013


WAFUGAJI wa kabila la Kimaasai wametakiwa kuuza mifugo na kusomesha watoto wao ili wapate elimu itakayowawezesha kupata fursa mbalimbali za kiuchumi ,kijamii na kisiasa  kama jamii zingine hapa nchini.
Wito huo ulitolewa na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari katika harambee ya ujenzi wa shule ya Sekondari katika eneo la Ngabobo Wilayani Arumeru.
Nassari alisema kuwa jamii hiyo ipo nyuma katika Nyanja za  kimaendeleo  kutokana na kuendelea na mfumo wa ufugaji wa kuhamahama jambo ambalo limesababaisha watoto wengi  katika jamii hiyo kukosa fursa ya kupata elimu.
“Nawasihi  ndugu zangu wamasai sasa muanze kuwekeza katika elimu kwa watoto wenu ,nyakati hizi hakuna njia nyingine ya kutatua changamoto ni elimu pekee ndio njia ya kuweza kuleta faida isiyokwisha katika maisha yenu”alisema Nassari.
Aidha Mbunge huyo aliwapongeza wananchi wa eneo hilo kwa kujitokeza kwa wingi na kutoa mifugo kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo na kusema kuwa huo ndio mwanzo mpaya wa jamii hiyo kuanza kubaduilika kwa dhati na kuthamini elimu.
Aliwaambia wafugaji hao kwamba jamii hiyo imekuwa ikitoa viongozi waadilifu na wachapa kazi akiwemo waziri Mkuu mstaafu Edward Moringe Sokoine na Edward Lowasa.
“Kwa asili mmejaliwa kuwa na watu wenye mismamo na maamuzi yenye masilahi kwa umma ,wasomesheni watoto wenu ili waweze kutoa mchango katika kujenga taifa letu katika nynaja za kiuchumi na hata kisiasa”alisema Nassari.
Aliwaambia wafugaji hao kuwa yeye alisoma katika hali ngumu na wakati fulani akisoma shule ya sekondari wazazi wake walilazimika kuuza kabati la vyombo ili apate ada.
Alisema aliweza kusoma vizuri na kumaliza chuo kikuu ambapo sasa ana uwezo wa kununua kila nachokihitaji katika maisha yake na jamii yake.
Katika harambee hiyo wananchi walitoq ngombe zaidi ya 50 zenye thamani ya shilingi milioni 15 mbuzi na kondoo wenye tahamni ya shilingi milioni 7
Katika harambee iliyoendeshwa na mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Onesmo Nangole  kwa niaba ya  Waziri   Mkuu mstaafu Edward Lowasa jumla ya shilingi milioni 53 zilipatikana

MAJASUSI  wa shirikisho la ujasusi la nchini Marekani wamefika jijini Arusha kusaidiana na wapelelezi wa nchini Tanzania katika uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa bomu  kwa waumini wa kanisa katoliki na Balozi wa Vatican nchini siku ya jumapili. 

Magesa alitoa taarifa hiyo wakati akitoa taarifa ya Mkoa kwa waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alipozuru eneo la tukio na kuwatembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali na kuwapa pole.

Wakati maafisa hao wakifika jijini humo tayari vyombo vya usalama vinawashikilia watu zaidi ya 10 miongoni mwao wakiwemo watu wanne  kutoka Saudia Arabia ambao waliwasili nchini kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA) siku moja kabla ya tukio.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alisema kuwa watu hao walikamatwa muda mfupi wakiondoka  nchini kupitia mpaka wa Namanga kuelekea nchini  Kenya baada ya tukio kutokea.
Hata hivyo taarifa hiyo haikuweza kutoa ufafanuzi zaidi na kwamba taarifa zaidi juu ya upepelezi zitatolewa kadri muda na wakati utakavyoruhusu.
Paroko wa Parokia ya Olasiti akitoa taarifa kwa waziri Mkuu mstaafu Eward Lowasa
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa kanisa katoliki katika eneo lilipotokea mlipuko wa bomu

Monday, May 6, 2013

Askari wa JWTZ akiwasili katika eneo la tukio 

eneo bomu lilipolipuka 


Wananchi wakijaribu kufikiri kuhusu kilichotokea 

Ulinzi Mkali eneo lilipotokea mlipuko

WACHUNGUZI WA MILIPUKO WAKICHUNGUZA MABAKI YA MLIPUKO





IDADI, ya watu waliopoteza maisha katika shambulio la wa bomu ililolipuka katika sherhe za uzinduzi wa kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Yosef Olasiti imeongezeka na kufikia wawili.

Majeruhi aliyefariki jana usiku ametambuliwa kuwa ni James Gabriel (16) 

Hali kadhalika majeruhi wwengine hali zao ni mbaya na wapo katika chumba cha uangalizi maalum katika hospitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru.

Hadi asubuhi ya leo hakuna majeruhi walioruhusiwa kurudi nyumbani  na majeruhi mmoja alikimbizwa jana katika hospitali ya rufaa ya KCMC  Mkoani Kilimajaro.

Wakati huo huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Gharib Bilal na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini  Inspekata Jenerali  Said Mwema wamewaasili Jijijni Arusha na kuwatembelea majeruhi wa bomu ililolipuka katika sherhe za uzinduzi wa kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Yosef Olasiti.

 lililolipuliwa kati kati ya waumini wa wa kanisa Katoliki la Parokia ya Mtakatifu Joseph na kusababaisha kifo cha mtu mmoja na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa vibaya.

Dr.Bilal aliwasili katika hospitali ya Mkoa wa  wa Arusha Mount Meru akiongozana na Mkuu wa kanisa la kiiinjili la Kilutheri Dr,Alex Malausa pamoja na viongozi wa madhehebu kadhaa ya dini Mkoani Arusha.

Akizungumza na majeruhi hao Makamu wa Rais aliwahakikishia majeruhi hao kuwa serikali itatumia nguvu  zote  za ulinzi na usalama kuwatia mbaroni watuhumiwa wa tukio hilo.

Wakati huo huo watu sita wanashikiliwa na polisi kufuatia tukio hilo ambalo kwa mara ya kwanzalinatarajiwa kuongeza hofu na mashaka juu ya usalama kwa wananchi  hasa katika mikusanyiko na sehemu za kupata huduma mbalimbali za kijamii.

Sunday, May 5, 2013


A bomb blast hit a Catholic church on Sunday in Arusha in northern Tanzania, killing one person and leave 60 people  injured .

The dead was among the church followers who were gathering for Sunday prayers identified as Regina Loningo.

The church located in Arusha's Olasiti suburb was bombed just before a mass in the presence of Bishop  Josephat Louis Lebulu of Arusha Diocese, who was accompanied by a representative of Pope of Vatican.

Police in Arusha said one man was arrested in connection with the incident, which caused a lot of panic in the tourist capital of the East African country.

Casualties are yet to be updated. "We are still working on the matter. We'll give more detail after investigating the matter," said Arusha Regional Police Commander Liberatus Sabas.
He said the man was arrested following a tip-off from people at the scene when the explosion occurred.

"We are still interrogating the suspect," he said.
Regional Commissioner Magesa Mulongo described the blast as horrific and unique in Tanzanian history, calling on the public to remain calm.
"So, people should continue with their daily activities, as police and other security organs have normalized the situation," Mulongo said.
A witness said, "I saw more than 30 people, taken by a police vehicle, which took them to the Mount Meru Regional Hospital."
Another witness said the bomb hit the church at around 10:00 a. m. local time when church followers were gathering for the historic Sunday prayer at the new church.
"We were trying to organize ourselves for the mass, when we heard loud sound, the situation that made more people to start rushing out of the church," a witness told Xinhua.
This is the first bomb explosion at the church in the northern safari capital of Arusha.

Majeruhi wakiwa wamelala chini nje ya kanisa la Mtakatifu Joseph Olasiti Arusha
MAJERUHI 

SEHEMU BOMU  LILIPOLIPUKA
MANESI NA MADAKTARI WAKIHUDUMIA MAJERUHI 


Habari zilizopatikana hivi punde zinaeleza kuwa kumetokea mlipuko wa kitu kinachodhaniwa kuwa bomu katika Parokia mpya ya OLasiti  katika jimbo kuu la Arusha ambayo ilikuwa inazinmduliwa rasmi.

 Inaelezwa na baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo lililotokea saa tano kasoro asubuhi kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa na wamekimbizwa hospitali kupata matibabu.

kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Arusha Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mpaka sasa hakuna mtu aliyepoteza maisha kufuatia tukio hilo.

"Mlipuko umetokea vyombo vya usalama vipo hapa kufanya uchunguzi ,ninachoweza na mtu mmoja amepoteza maisha. 

Alisema kuwa watu 42 wamejerihiwa vibaya na polisi wanamshikilia mtu mmoja ambaye polisi wanasema wanamhoji kuhusu tukio hilo.

Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa bomu hilo lilirushwa na watu waliofika karibu na kanisa hilo wakivalia nguo za kuficha nyuso wakiwa katika gari ambayo namba zake hazikuweza kufamika na kurusha kitu ambacho kililipuka karibu na meza ya misa takatifu.

Misa hiyo ilikuwa inaendeshwa na Balozi  wa Vatican na mjumbe maalum wa Papa nchini Tanzania  Francisco Padila .

hadi kufika saa 8 mchana watu 42 walikuwa  wamejeruhiwa ibaya  katika ibada hiyo.

Mtu mmoja aliyetajwa kuwa ni Regina Loningo Kuresoi amepoteza maisha katika tukio hilo.

Maafisa wa jeshi la polisi ,askari wa jeshi la wananchi kikosi cha mabomu wapo katika eneo la tukio.


Time Management

Translator

Popular Posts

Fellow Bloggers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews