IDADI, ya watu waliopoteza maisha katika shambulio la wa bomu
ililolipuka katika sherhe za uzinduzi wa kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu
Yosef Olasiti imeongezeka na kufikia wawili.
Majeruhi aliyefariki jana usiku ametambuliwa kuwa ni James Gabriel (16)
Hali kadhalika majeruhi wwengine hali zao ni mbaya na wapo
katika chumba cha uangalizi maalum katika hospitali ya Mkoa wa Arusha Mount
Meru.
Hadi asubuhi ya leo hakuna majeruhi walioruhusiwa kurudi
nyumbani na majeruhi mmoja alikimbizwa jana
katika hospitali ya rufaa ya KCMC Mkoani
Kilimajaro.
Wakati huo huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr.Gharib Bilal na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekata Jenerali Said Mwema wamewaasili Jijijni Arusha na
kuwatembelea majeruhi wa bomu ililolipuka katika sherhe za uzinduzi wa kanisa
Katoliki Parokia ya Mtakatifu Yosef Olasiti.
lililolipuliwa kati
kati ya waumini wa wa kanisa Katoliki la Parokia ya Mtakatifu Joseph na
kusababaisha kifo cha mtu mmoja na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa vibaya.
Dr.Bilal aliwasili katika hospitali ya Mkoa wa wa Arusha Mount Meru akiongozana na Mkuu wa
kanisa la kiiinjili la Kilutheri Dr,Alex Malausa pamoja na viongozi wa
madhehebu kadhaa ya dini Mkoani Arusha.
Akizungumza na majeruhi hao Makamu wa Rais aliwahakikishia
majeruhi hao kuwa serikali itatumia nguvu
zote za ulinzi na usalama kuwatia
mbaroni watuhumiwa wa tukio hilo.
Wakati huo huo watu sita wanashikiliwa na polisi kufuatia
tukio hilo ambalo kwa mara ya kwanzalinatarajiwa kuongeza hofu na mashaka juu
ya usalama kwa wananchi hasa katika
mikusanyiko na sehemu za kupata huduma mbalimbali za kijamii.
0 comments:
Post a Comment