WAFUGAJI
wa kabila la Kimaasai wametakiwa kuuza mifugo na kusomesha watoto wao ili
wapate elimu itakayowawezesha kupata fursa mbalimbali za kiuchumi ,kijamii na
kisiasa kama jamii zingine hapa nchini.
Wito huo ulitolewa na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki
Joshua Nassari katika harambee ya ujenzi wa shule ya Sekondari katika eneo la
Ngabobo Wilayani Arumeru.
Nassari alisema kuwa jamii hiyo ipo nyuma katika Nyanja
za kimaendeleo kutokana na kuendelea na mfumo wa ufugaji wa
kuhamahama jambo ambalo limesababaisha watoto wengi katika jamii hiyo kukosa fursa ya kupata
elimu.
“Nawasihi ndugu zangu
wamasai sasa muanze kuwekeza katika elimu kwa watoto wenu ,nyakati hizi hakuna
njia nyingine ya kutatua changamoto ni elimu pekee ndio njia ya kuweza kuleta
faida isiyokwisha katika maisha yenu”alisema Nassari.
Aidha Mbunge huyo aliwapongeza wananchi wa eneo hilo kwa
kujitokeza kwa wingi na kutoa mifugo kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo na
kusema kuwa huo ndio mwanzo mpaya wa jamii hiyo kuanza kubaduilika kwa dhati na
kuthamini elimu.
Aliwaambia wafugaji hao kwamba jamii hiyo imekuwa ikitoa
viongozi waadilifu na wachapa kazi akiwemo waziri Mkuu mstaafu Edward Moringe
Sokoine na Edward Lowasa.
“Kwa asili mmejaliwa kuwa na watu wenye mismamo na maamuzi
yenye masilahi kwa umma ,wasomesheni watoto wenu ili waweze kutoa mchango
katika kujenga taifa letu katika nynaja za kiuchumi na hata kisiasa”alisema
Nassari.
Aliwaambia wafugaji hao kuwa yeye alisoma katika hali ngumu
na wakati fulani akisoma shule ya sekondari wazazi wake walilazimika kuuza
kabati la vyombo ili apate ada.
Alisema aliweza kusoma vizuri na kumaliza chuo kikuu ambapo
sasa ana uwezo wa kununua kila nachokihitaji katika maisha yake na jamii yake.
Katika harambee hiyo wananchi walitoq ngombe zaidi ya 50
zenye thamani ya shilingi milioni 15 mbuzi na kondoo wenye tahamni ya shilingi
milioni 7
Katika harambee iliyoendeshwa na mwenyekiti wa chama cha
Mapinduzi Mkoa wa Arusha Onesmo Nangole
kwa niaba ya Waziri Mkuu
mstaafu Edward Lowasa jumla ya shilingi milioni 53 zilipatikana
0 comments:
Post a Comment