MAJASUSI wa shirikisho la ujasusi la nchini Marekani
wamefika jijini Arusha kusaidiana na wapelelezi wa nchini Tanzania katika
uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa bomu kwa waumini wa kanisa katoliki na Balozi wa
Vatican nchini siku ya jumapili.
Magesa alitoa taarifa hiyo
wakati akitoa taarifa ya Mkoa kwa waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mizengo Pinda alipozuru eneo la tukio na kuwatembelea wagonjwa
waliolazwa katika hospitali mbalimbali na kuwapa pole.
Wakati maafisa hao wakifika
jijini humo tayari vyombo vya usalama vinawashikilia watu zaidi ya 10 miongoni mwao
wakiwemo watu wanne kutoka Saudia Arabia
ambao waliwasili nchini kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro(KIA) siku moja
kabla ya tukio.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa
Mulongo alisema kuwa watu hao walikamatwa muda mfupi wakiondoka nchini kupitia mpaka wa Namanga kuelekea
nchini Kenya baada ya tukio kutokea.
Hata hivyo taarifa hiyo
haikuweza kutoa ufafanuzi zaidi na kwamba taarifa zaidi juu ya upepelezi
zitatolewa kadri muda na wakati utakavyoruhusu.
Paroko wa Parokia ya Olasiti akitoa taarifa kwa waziri Mkuu mstaafu Eward Lowasa |
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa kanisa katoliki katika eneo lilipotokea mlipuko wa bomu |
0 comments:
Post a Comment