Hospitali
ya Misheni ya Kolandoto katika Wilaya Shinyanga mjini inakabiliwa na changamoto kubwa ya
kuwahudumia watu waisho na virusi vya
ukimwi kufuatia kukosekana kwa mashine ya kuhesabu kinga za mwili (CD4) katika
hospitali hiyo.
Mashine hiyo inaelezwa na
wataalamu wa tiba kujua kinga za mwili
za mwathirika wa virusi vya ukimwi ili kujua iwapo anastahili kuanzishiwa dawa
za kupunguza makali ya ugonjwa wa ukimwi ARV.
Akizungumza na waandishi wa habari
waliotembelea hospitali hiyo juzi, Kaimu Mganga Mkuu Dr.Phares Bwire alieleza kuwa ukosefu wa mashine hiyo umekuwa ukisababaisha kuharibika
kwa sampuli za damu ambazo zinalazimika kuplekwa hospitali ya Mkoa wa Shinyanga kwa vipimo
zaidi.
Alisema hospitali hiyo ilipata
msaada wa mashine mbili za kupima damu (Screen Master na Full Blood Picture)
kutoka Shirika la Afya linalojishughulisha na vita dhidi ya Ukimwi na Utoaji wa
Huduma za Kujikinga, Matunzo na Tiba kwa wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi
(AGPAHI).
“Tunakabiliwa na changamoto katika
utoaji wa huduma kwa Waviu naomba wadau
wengine wajitokeze kutusaidia kama walivyofanya shirika la afya linalojishughilisha na
mapambano ya ukimwi ,tiba na matunzo kwa
wagonjwa wa ukimwi AGPAHI… ukosefu wa mashine hii muhimu ya kuhesabu CD4 unasababisha kuharibika kwa
baadhi ya sampuli za damu.
Alisema kuwa wakati mwingine
majibu ya CD4 yanachelewa kufika ambapo
wanalazimika kusubiri kwa siku zisizopungua 14 hadi mwezi mmoja jambo
linalowafanya wagonjwa kukata tamaa na wengine kukimbia matibabu
Kwa mujibu wa mganga huyo huduma
za kupima na kutoa dawa za ARV kwa waathirika wa VVU zilianzishwa hospitalini
hapo mwaka 2007 kwa ushirikiano na
shirika la AGPAHI.
Mganga huyo alisema mbali na
msaada wa mashine hizo, AGPAHI imewezesha mafunzo kwa watoa huduma wa kliniki
za waathirika wa VVU, watoa hduma majumbani, vitendanishi, ukarabati wa majengo
na dawa za ARV.
“Tangu tumeanza na shirika hili
mpaka sasa ni zaidi ya sh milioni 200 za AGPAHI zimetumika kwenye shughuli
mbalimbali hospitalini hapa hivyo tunaomba na mashirika mengine wajitokeze
kutusaidia maana wagonjwa ni wengi,” alisema Dk. Phares.
Awali alibainisha kwamba hadi sasa
waathirika zaidi ya 831 wanahudumiwa hospitalini hapo kwa dawa na ushauri huku
akibainisha kwamba kati ya waathirika hao 70 ni watoto chini ya miaka 14 ambapo
waathirika 114 wanatumia dawa za ARV wakati watoto wanaopewa dawa hizo ni 39.
Mwisho…
0 comments:
Post a Comment