Sunday, April 21, 2013


WAFANYABIASHARA zaidi ya 300 wa maduka yaliyopo katika stendi ndogo Jijini   Arusha wamegoma kulipa kodi mpya ya pango iliyotolewa na halamashauri ya Jiji hivi karibuni.
Wafanyabiashara hao wamedai kuwa  uongozi wa  Jiji  la Arusha umetoa  mkataba mpya na kiwango cha juu cha kodi ambayo sio halalali .
Kwa mujibu wa mkataba huo mpya wafanyabaishara hao wanatakiwa kupipanshilingi 275,000 kwa mwezi badala ya shilingi  60,000 wanazolipa siku zote.
Katibu wa wafanyabiashara hao Melance Kisoka alisema kuwa manispaa hiyo pia imefanya makosa ya kisheria kwa kutengeneza mkataba  mpya na kupandisha kodi  kwa kiwango cha juu ambacho hakiwezi kulipika.
“Hatufahamu ni wapi wametoa haya mahesabu kwamba tulipe kiasi hiki cha fedha na pia wameweka mktaba w amiezi minne  hali ambayo kabisa ni kinyume na hali ya mazingira ya biashara na taasisi zinazotoa mikopo utawezaje kukopa pesa na kufanya biashara uweze kurejesha mkopo hakuna benki itakayoweza kukubali kitu kama hichi”alisema Kisoka
“Kwanza ieleweke wazi hatupingi kulipa kodi lakini kuna mambo ya msingi yanapaswa kuwekwa sawa ,moja ni kuweka bayana mmiliki halali  wa maduka kwa kuwa haya maduka tuliyajenga wenyewe ”alisema Kisoka.
Mfanyabiashara mwingine  Abraham  Chipaka  alisema kuwa hatua hiyo ni mbinu  chafu za manispaa ya jiji kutaka kuwapora maduka yao waliyojenga kwa nguvu zao.
“Hawa Manispaa tumewagundua na mbinu zao chafu wanachotaka ni kutupora maduka yetu lesema kuwa wao wakiwa wadau muhimu katika suala hilo.
Naye Betty Manjira alisema kuwa wanashangazwa na manispaa kuongeza kodi   kubwa wakati  hakuna huduma zozote katika kituo hicho ikiwemo huduma ya choo.
“Humu ndani wanatudai kodi lukuki ,usafi ,maegesho hizi kodi zinaenda wapi?nchi zingine watu wanalipa kodi na kufaidi matunda ya kodi zao hapa kwetu kuna nini”alihoji Manjira
Tito Isack Zumba akichangia katika mjadala huo alisema kuwa walipewa kibali cha kujenga mwaka 1994 lakini katika mkataba huo hakuna sehemu inayoonyesha  mmiliki wa wa jengo  ni nani.
Mfanyabiashara mwingine Dominick Mollel alisema kuwa inashangaza kwao kuona manispaa inataka kuwapora maduka yao wakati manispaa hiyo hiyo imewamilikisha  wafanyabaishara wenzao  vibanda  eneo la Krokon.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Afwilile Lamsy  kwa kifupi  alisema kuwa walichukua hatua hiyo kwa kuzingatia hali ya biashara   ilivyo katika eneoi hilo.
Alisema kuwa atalitolea ufafanuzi suala hilo wiki hii mbele ya vyombao vya habari.
MWISHO……………………………………

1 comment:

  1. Nimefuatilia kwa makini kuhusu kutoelewana kati ya Halmashauri ya jiji la Arusha na wafanyi biashara. Iweje wafanya biashara wa stendi ya vifodi Arusha wajenge vibanda vya biashara halafu halmashauri ya jiji Arusha idai kua ni mali yake.Huu ni uporaji na wizi mtupu.Si halali kwa wafanyibiashara kulipa kodi ya pango ila wanachotakiwa kulipa ni kodi ya ardhi kama wenzao wa Krokon.Na sio nia ya serikali kufanya haya yanayofanywa bali ni ubinafsi wa baadhi ya wafanyakazi na baadhi ya madiwani kwa chuki za kisiasa zinazoendelea hapa Arusha.Ni nia njema ya serikali kusaidia wajasiria mali si kuwapora na kuongeza bei ya pango kwa asilimia karibu mia tano. Halmashauri ielewe wazi kua wao ni chombo cha serikali na hawatakiwi kuingiza mambo ya chuki za kisiasa na ubinafsi katika taasisi ya serikali.Na serikali haifanyi biashara. Leo sio karne ya kudanganyana na kutumia ujanjaunja kwa mambo yaliyo wazi. Ningewashauri halmashauri ya jiji la Arusha kuacha mara moja haya mambo ambayo yaipaka matope vyombo vya serikali mbele ya wananchi. Nawasihi viongozi wa serikali walioko madarakani kwa sasa wasiachie hili jambo likaendelea kuleta mfarakano kati ya wananchi na serikali hapa Arusha.

    ReplyDelete

Time Management

Translator

Popular Posts

Follow by Email

Fellow Bloggers

Google+ Followers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews