FAMILIA ya marehemu
Baba skofu Thomas Laizer wa Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania
dayosisi ya kaskazini kati imesema kuwa hayati Baba askofu ameacha wosia mzito
kwa waumini, wachungaji na viongozi wa kanisa hilo baada ya yeye kupita.
Akizungumza nyumbani kwa askofu huyo katika eneo la Nduruma
mke wa askofu huyo Mama Maria Laizer alisema kuwa mume wake kila mara alikuwa
anasisitiza kuwa kazi aliyoianzisha iendelezwe na isiharibiwe kwa vyovyote
vile.
“Baba askofu alisisitiza
jambo hili hata kwa wote waliofika kumjulia hali akiwa kitandani kwake kuwa
wahakikishe kuwa kazi aliyoianza inaendelezwa “alisema Mama Laizer.
Alileza kuwa alikuwa na mume wake masaa machache kabla ya
kifo chake na kwamba mchana wa siku aliyoaga dunia alikuwa na hali nzuri lakini
baadye hali yake ilibadilika na kuondokewa na uhai.
Alisema kuwa askofyu huyo alianza kusumbuliwa na maradhi ya
kansa kwa kipindi cha miaka minne iliyopita lakini hakuweza kupata tiba stahili
kwa haraka.
“Alikuwa akilalamika maumivu katika tumbo lake mara kwa mara
na baadaye alizidiwa tukampeleka Nairobi akatibiwa lakini baada ya muda alianza
tena kulalamika maumvu na ndipo akapelekwa India na kugundulika kuugua kansa
ambayo tayari ilikuwa imesambaa mwilini”alisema Mama Laizer.
Marehemu Baba askofu Thomas Laizer ameacha mjane watoto wanne
na mjukuu mmoja.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
0 comments:
Post a Comment