Askofu wa
kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania
dayosisi ya kaskazini kati Askofu Thomas lazier amefariki Dunia jioni ya
leo.
Habari ambazo
zimethibitishwa na katibu Mkuu wa dayosisi hiyo Israel Ole Karyongi zimesema
kuwa askofu alikumbwa na mauiti majira ya saa
12 za jioni ya leo.
“Ni kweli
baba Askofu amepita na tuko katika hali ya dharura ngumu na tungependa mtuachie
nafasi ili tuwape taarifa juu ya msiba huu kesho”alisema Karyongi akizungumza kwa
njia ya simu .
Askofu lazier
ndiye askofu wa kwanza wa na mwanzilishi
wa dayosisi hiyo ambayo awali ilikuwa
ikiitwa dayossi Mkoani Arusha kabla ya mwaka juzi kubalishw ajina na kuitwa dayosisi
ya kaskazini kati.
Ni msiba
mkubwa mno katika Mkoa wa Arusha kutokana na askofu huyo kupata umaarufu katika kazi zake za kiroho na
kijamii husasan jamii ya kabila la wamasai.
Anatajwa kushiriki
katika kuendeleza jamii hiyo kielimu kwa kubuni na kuanzisha shule zaidi ya
ishirini za sekondari zikiwemo maalum kwa ajili ya watoto wa kike.
kufuatia msiba huo,Waziri Mkuu mstaafu Edward Ngoyai Lowasa amesema kuwa kanisa na jamii limempoteza kiongozi na mpigania maendeleo ya jamii kiroho na kimwili.
“Tumepoteza
kiongozi wa kiroho na kijamii,amehusika katika kuelimisha jamii kwa kuanzisha
shule nyingi za Sekondari,amehusika pia ujenzi wa hospitali ya rufaa ya Arusha
Lutheran Medical Center,zahanti na vituo vya afya katika vijiji kadhaa Mkoani Arusha pamoja na hoteli ya Corridor springs”alisema
Lowasa.
Aliwataka waumini wa kanisa la KKKT kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu baada ya kuondokewa na kiongozi wao.
Aidha aliwapongeza madaktari wa hospitali ya Seliani kwa jitihada zao za kumsaidia baba askofu akiendelea na matibabu katika hospitali hiyo.
0 comments:
Post a Comment