__ |
Mkurugenzi wa TACTO Freddy Massawe akijibu maswali yaa waandishi wa habari hawaonekani katika picha |
Mkurugenzi mtendaji wa chama cha wafanyabiashara wa utalii wa kitamaduni nchini(TACTO) Fred Massaweakionyesha moja ya picha za wachoraji kutoka Tanzania zitakazoonyeshwa katika tamasha kigali |
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi
mtendaji wa chama cha wafanyabiashara wa utalii wa kitamaduni nchini(TACTO)
Fred Massawe alisema kuwa tamasha hilo litafanyika mwezi huu.
Ameeleza kuwa tamasha hilo linalenga kuunganisha
wananchi wa jumuiya ya afrika mashariki na litakuwa linafanyika kwa mzunguko
katika nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Alisema kuwa washiriki wa tamasha hilo watakuwa ni
wachoraji wachonga vinyago ,ngoma za kitamaduni na washonaji wa shanga na
bidhaa mbalimbali zenye sura za kitamaduni.
Akilezea zaidi alisema kuwa utalii wa kitamaduni
unaweza una uwezo mkubwa wa kjuinua uchumi wa hata mtu mmoja mmoja.
Alisema kuwa utalii wa kitamaduni unakadiriwa
kuongeza ajira zaidi ya laki moja na kama juhudi za kuutangaza zikifanyika
ajira hizo zinaweza kuongezeka maradufu.
Alitoa wito kwa wadau wa utalii na serikali na wadau wengine kusaidia kuwezesha kupeleka
watu wengi zaidi katika tamasha hilo kutokana na nchi kujaa utajiri wa tamaduni
zenye kuvutia.
Alisema kuwa Tanzania ina umuhimu mkubwa wa
kushiriki tamasha hilo kutokana na kuwa tamaduni nyingi na vivutio vingi vya
asili ambavyo vitaitangaza nchi katika masoko ya utalii.
Mwisho……………….
0 comments:
Post a Comment