Sunday, April 28, 2013

SERIKALI imewataka viongozi  wa dini kuwa mstari wa mbele kuhimiza utunzaji wa mazingira kwa waumini wao ikiwa  ni harakati za kuzuia uharibifu wa mazingira  kwa kupanda miti  ya asili  inayotunza mazingira .

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Nyerembe Munasa wakati akizungumza na wananchiw a Arumeru kata ya Akheri Tengeru ,wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya mradi wa utunzaji wa mazingira baina ya watanzania wa Tengeru na nchi ya Polland mradi unaojulikana kama  Tengeru Leominster Natural  Resource Conservation Project (TLNRCP).

Munasa anasema kuwa  mazingira ni uhai yanapaswa kutunzwa na hivyo Viongozi wa dini wanatakiwa kutumia muda wao kupiga vita waharibifu wa mazingira kwa kuwahubiria kuhusu madhara yanayotokana   na kuharibu mazingira .

Aidha alipongeza jitihada za Chuo cha Mafunzo ya Mifugo kwa kushirikiana na wadau wa mazingira kutoka Uingereza wakiwa wanaongozwa na Barbara Woodward kutoka Uingereza na kufanikiwa kwa pamoja  kutunza mazingira na kusaidia ustawi wa maisha ya wakazi wa Tengeru na majirani .

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Vyuo vya Mafunzo  ya Mifugo Tanzania
 Endrick Kapinga alisema kuwa zoezi hilo limeweza kufanikiw a kutokana na ushirikiano baina ya wananchi wa Tanzania  Tengeru na Uingereza
Kapinga alisema  ,na kuwa Tengeru  imeweza kuwa mfano wa utunzaji wa mazingira kwa kipindi cha miaka 25 na kufanya wenyeji kwenda kujifunza Chuo hapo ,ambapo wanajifunza namna ya kutunza na kuhifadhi mazingira
Mkurugenzi huyo aliomba mradi huo utunzwe ikiwa ni pamoja na kutambuliwa na kuendeleza na Wizara ya Mifugo na maendeleo ya Uvuvi,Wizara ya elimu  na mafunzo ya ufundi ,Wizara ya Afya  na wadau wengine wa maendeleo ,kutokana na ukweli kuwa mradi huo pia ulihusika na kutoa elimu katika Nyanja mbali mbali na Afya .


Kapinga ameomba Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Mafunzo Tengeru Elly Masam ,kuendeleza mradi huo kwa kuhakikisha miti ya iliyopandwa inatunzwa na kukabiliana na watu wenye nia ya kuharibu mazingira hayo

0 comments:

Post a Comment

Time Management

Translator

Popular Posts

Follow by Email

Fellow Bloggers

Google+ Followers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews