Sunday, April 28, 2013





SERIKALI imewataka viongozi  wa dini kuwa mstari wa mbele kuhimiza utunzaji wa mazingira kwa waumini wao ikiwa  ni harakati za kuzuia uharibifu wa mazingira  kwa kupanda miti  ya asili  inayotunza mazingira .

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Nyerembe Munasa wakati akizungumza na wananchiw a Arumeru kata ya Akheri Tengeru ,wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya mradi wa utunzaji wa mazingira baina ya watanzania wa Tengeru na nchi ya Polland mradi unaojulikana kama  Tengeru Leominster Natural  Resource Conservation Project (TLNRCP).

Munasa anasema kuwa  mazingira ni uhai yanapaswa kutunzwa na hivyo Viongozi wa dini wanatakiwa kutumia muda wao kupiga vita waharibifu wa mazingira kwa kuwahubiria kuhusu madhara yanayotokana   na kuharibu mazingira .

Aidha alipongeza jitihada za Chuo cha Mafunzo ya Mifugo kwa kushirikiana na wadau wa mazingira kutoka Uingereza wakiwa wanaongozwa na Barbara Woodward kutoka Uingereza na kufanikiwa kwa pamoja  kutunza mazingira na kusaidia ustawi wa maisha ya wakazi wa Tengeru na majirani .

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Vyuo vya Mafunzo  ya Mifugo Tanzania
 Endrick Kapinga alisema kuwa zoezi hilo limeweza kufanikiw a kutokana na ushirikiano baina ya wananchi wa Tanzania  Tengeru na Uingereza
Kapinga alisema  ,na kuwa Tengeru  imeweza kuwa mfano wa utunzaji wa mazingira kwa kipindi cha miaka 25 na kufanya wenyeji kwenda kujifunza Chuo hapo ,ambapo wanajifunza namna ya kutunza na kuhifadhi mazingira
Mkurugenzi huyo aliomba mradi huo utunzwe ikiwa ni pamoja na kutambuliwa na kuendeleza na Wizara ya Mifugo na maendeleo ya Uvuvi,Wizara ya elimu  na mafunzo ya ufundi ,Wizara ya Afya  na wadau wengine wa maendeleo ,kutokana na ukweli kuwa mradi huo pia ulihusika na kutoa elimu katika Nyanja mbali mbali na Afya .


Kapinga ameomba Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Mafunzo Tengeru Elly Masam ,kuendeleza mradi huo kwa kuhakikisha miti ya iliyopandwa inatunzwa na kukabiliana na watu wenye nia ya kuharibu mazingira hayo

Thursday, April 25, 2013


Jeshi la polisi linamsaka Mbunge wa Jimbo la Arusha Godbless Lema kwa tuhuma za kuhusika katika vurugu zilizotokea juzi katika chuo cha Uhasibu Mkoani Arusha  na kusababisha chuo hicho kufungwa kwa muda usiojulikana.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Arusha Kamishna msaidizi wa Jeshi la polisi Ibrahim Kilongo aliwaaambia waandishi habari kuwa jeshi hilo limetoa ilani kwa mbunge huyo kujisalimisha polisi haraka.

“Tunamtaka popote alipo afike mwenyewe  poilisi na bado tunaendelea kumtafuta popote  alipo ,ni muhimu afike tufanye naye mahojiano kuhusu yaliyotokea katika chuo cha uhasibu ”alisema Kilongo.

Kaimu kamnda huyo alikataa kutaja majina ya wanafunzi kadhaa waliokuwa wamekamatwa katika vurugu hizo.

“Tutawapa hayo majina ya wanafunzi tuliwakamata katika tukio hilo  baadaye  kwa sasa tunaendelea kuwahoji ili kupata taarifa muhimu za vurugu zilizotokea  “alisema Kamanda huyo kwa kifupi.

Inadaiwa  kuwa Lema anatuhumiwa kuhusika katika vurugu zilizopekea kudhalilishwa na kuzomewa kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.

Mara baada ya kutulizwa kwa vurugu hizo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mgesa Mulongo aliliagiza jeshi l polisi kumkamata Mbunge huyo  kwa kile kilicholezwa kuwa ni kumhusiha na vurugu zilizotkea chuoni hapo.

Hata hivyo Mbunge huyo alikana vikali kuhusika katika vurugu zozote na kueleza kuwa alitumia nafasi yake kuwashawishi wananfunzi kurudi chuoni na kisha akawasiliana na Mkuu wa Mkoa kufika kuzungumza na wanafunzi hao.

Katika tukio hilo  lililosababisha mabomu ya machozi kurindima kwa kwa muda katika viunga vya chuo hicho Mkuu huyo wa Mkoa alijikuta akizomewa baada ya kushindwa kuhutubia mamia ya wanafunzi baada ya kukosekana kwa kipaza sauti.

Awali wanafunzi hao walitaka kuandamana kuelekea kituo  kikuu cha polisi Jijini hapa kufuatia mwanafunzi mwenzao kuuawa katika mazingira waliyodai yana utata karibu na chuo hicho usiku wa kuamkia siku ya  jumatano wiki hii.

Baadhi ya wananchi waliohojiwa na gazeti hilo kutoka maeneo ya Njiro Peter Muinisi na Fredy Swat walisema kuwa wameshangazwa na hatua ya Mkuu wa Mkoa kumnyooshea Lema kidole na kuagiza akamatwe kuhusiana na tukio hilo.

“Hii ni aibu tulimwona Lema akiwabembeleza wanafunzi wasiandamane  kwenda kati kati ya mji  ,alitaka jambo hilo litafutiwe ufumbuzi bila kuleta madhara yoyote,hebu fikiri wanafunzi wale wangefika kati kati ya mji hali ingekuwaje”alihoji Muinisi.

Aidha alisema viongozi wanapaswa kuheshimiana na kutenda kazi bila kuweka sababu za kibinafsi katika mambo ambayo majibu yake yako wazi mbele ya umma na kutengeneza picha mbaya kwa viongozi.

Sunday, April 21, 2013


MORE  than 300 shop traders  in Arusha city trading  along the local minibus stand  have refused  to pay a new rent tax imposed by the council , claiming that  the  the recent new  agreement  is not legally valid and the tax is too high to afford.
Through their union meeting which was held yesterday the traders said the municipal tax raised from Shs 60,000Tsh per month  to TShs 275,000 without their views or  negotiation was is illegal and it is against the spirit of  good governance policy in the country
The General Secretary of the traders and shop owners association Melance Kisoka said both the new tax and the agreement are illegal and show a secret motive of the council to steal their shops which they built at their own costs.
“How can this be possible to inflate tax beyond deadly proportion, is it really our government doing all these to us ,they want our children to starve and fail to go to school, this is our means for  survival  we will fight until justice is done “Said Kisoka
He said his association members have never refused  to pay  council   taxes but participation and negotiation are the  key matters to dictate how much should be paid regarding on their business environment.  
He said the council distributed new rent agreement to the traders forcing them to sign the new agreement before Wednesday this week something that has terribly shocked the traders.
  Kisoka  said that the new contract has not laid  down some  important facts one being the clear indication of the premises ownership and also its period  is too shot  leading to failure of  business plans and  don’t comply with financial and loaning  institutions the country.
Another trader interviewed by this paper  Abraham Chipaka said that the move is dirty tricks of the municipality of the city to  grab  their shops  which they tokk loans from banks  and  build more than 15 years  ago.
"This is a sign of rejection to majority poor for the interest of the few rich and in power, we will use every means possible to retain our properties and our constitutional right to be heard and given our right as bonafide citizens of this country “He said
On her part Betty Manjira lamented on the municipal move to impose new and high  taxes saying there is no any services at the center including toilet service, water and other important services
“In other countries  of the World people enjoy paying taxes because they see what their money has done in terms of development projects and improved services  but here in our Municipal  is totally different ,they collect and probably all disappear we have to change this culture by addressing issues like these “She said
Tito Isaac Zumba contributing to matter  said they were given permission by the town council 1994 in an agreement  which has not shown that the  premises erected belongs to the  authority their fore in his vew they are entitled to pay for land rent.
Dominick Mollel  said  it was a big surprise to  see the municipality seeks to take away a their stores instead of  helping them to develop their businesses to fasten development in the sector in creation of self employment  for the better of  the country and its people.
“I wonder why they want to steal in the day light ,surprisingly some other traders of Krokon area have been given shops which constructed by the council  free ,there is a political move here, we will stand to deny to the fullest “Said Mollel
Commenting on the matter Levolosi ward Councilor Ephata Nanyaro supported entrepreneurs   urging them to claim their rights anywhere without fear
He further said the full council meetings have never passed any bill to increase or impose new taxes to Stand Ndogo traders
.Asked about the issue Acting Director of Arusha Council Lamsy Afwilile maintained that his council acted under lawful directives and promised to convene a press conference to elaborate the matter in full details.

WAFANYABIASHARA zaidi ya 300 wa maduka yaliyopo katika stendi ndogo Jijini   Arusha wamegoma kulipa kodi mpya ya pango iliyotolewa na halamashauri ya Jiji hivi karibuni.
Wafanyabiashara hao wamedai kuwa  uongozi wa  Jiji  la Arusha umetoa  mkataba mpya na kiwango cha juu cha kodi ambayo sio halalali .
Kwa mujibu wa mkataba huo mpya wafanyabaishara hao wanatakiwa kupipanshilingi 275,000 kwa mwezi badala ya shilingi  60,000 wanazolipa siku zote.
Katibu wa wafanyabiashara hao Melance Kisoka alisema kuwa manispaa hiyo pia imefanya makosa ya kisheria kwa kutengeneza mkataba  mpya na kupandisha kodi  kwa kiwango cha juu ambacho hakiwezi kulipika.
“Hatufahamu ni wapi wametoa haya mahesabu kwamba tulipe kiasi hiki cha fedha na pia wameweka mktaba w amiezi minne  hali ambayo kabisa ni kinyume na hali ya mazingira ya biashara na taasisi zinazotoa mikopo utawezaje kukopa pesa na kufanya biashara uweze kurejesha mkopo hakuna benki itakayoweza kukubali kitu kama hichi”alisema Kisoka
“Kwanza ieleweke wazi hatupingi kulipa kodi lakini kuna mambo ya msingi yanapaswa kuwekwa sawa ,moja ni kuweka bayana mmiliki halali  wa maduka kwa kuwa haya maduka tuliyajenga wenyewe ”alisema Kisoka.
Mfanyabiashara mwingine  Abraham  Chipaka  alisema kuwa hatua hiyo ni mbinu  chafu za manispaa ya jiji kutaka kuwapora maduka yao waliyojenga kwa nguvu zao.
“Hawa Manispaa tumewagundua na mbinu zao chafu wanachotaka ni kutupora maduka yetu lesema kuwa wao wakiwa wadau muhimu katika suala hilo.
Naye Betty Manjira alisema kuwa wanashangazwa na manispaa kuongeza kodi   kubwa wakati  hakuna huduma zozote katika kituo hicho ikiwemo huduma ya choo.
“Humu ndani wanatudai kodi lukuki ,usafi ,maegesho hizi kodi zinaenda wapi?nchi zingine watu wanalipa kodi na kufaidi matunda ya kodi zao hapa kwetu kuna nini”alihoji Manjira
Tito Isack Zumba akichangia katika mjadala huo alisema kuwa walipewa kibali cha kujenga mwaka 1994 lakini katika mkataba huo hakuna sehemu inayoonyesha  mmiliki wa wa jengo  ni nani.
Mfanyabiashara mwingine Dominick Mollel alisema kuwa inashangaza kwao kuona manispaa inataka kuwapora maduka yao wakati manispaa hiyo hiyo imewamilikisha  wafanyabaishara wenzao  vibanda  eneo la Krokon.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Afwilile Lamsy  kwa kifupi  alisema kuwa walichukua hatua hiyo kwa kuzingatia hali ya biashara   ilivyo katika eneoi hilo.
Alisema kuwa atalitolea ufafanuzi suala hilo wiki hii mbele ya vyombao vya habari.
MWISHO……………………………………

Sunday, April 14, 2013


Mfanyabiashara Maarufu Mkoani Arusha Peter Joseph Mallya almaarufu Bob Sambeke amefariki dunia baada ya kuanguka na ndege yake binafsi muda mfupi kabla ya kutua katika uwanja mdogo wa ndege uliopo katika eneo la Magereza kilomita sita kutoka kati kati ya Jijiji la Arusha.

Kaimu kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Arusha kamishna msaidizi wa Polisi Ibrahim Kilongo alisema kuwa ajali jiyo ilitokea saa moja na nusu jioni.

Alisema kuwa marehemu Mallya alikuwa peke yake na ndiye amepoteza maisha na kuacha ndege hiyo ikiwa imeharibika vibaya kutokana na kuangukia miti mikubwa iliyokuwa katika eneo la ajali.

“Ni kweli ajali imetokea na tayari mwili wa marehemu upo katika chumba cha kuhifadhi maiti ukisubiri taratibu za familia yake za mazishi”alisema Kilongo.

Alisema kuwa chanzo kamili cha jail hiyo bado hakijafahamika na kwamba uchunguzi utaendeshwa na vyombo vya usalama na mambo ya anga ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Hata hivyo habari ambazo bado hazijathibitishwa kutoka kwa maafisa wa mtandao wa kuongozea ndege uwanjani hapo zinasema kuwa marehemu alikatazwa kutua na ndege yake katika wakati huo lakini haifahamiki ni kwanini hakufuata ushauri huo.

Ajali  hiyo ni ya pili kutokea karibu na uwanja huo baada ya mwaka 1998 kutokea kwa ajali ambayo iliua watu sita baada ya ndege ndogo aina ya cesna kuanguka kati kati ya shamba la kahawa katika eneo hilo.




Friday, April 12, 2013

THE government has urged charitable organizations   operating   various projects in different communities to ensure that all groups in the society are able to benefit from their donations regardless of race and religion they come from.

The call was made by the Arumeru District commissioner Nyirembe Munasa at the launch of shoes distribution to 36,000 pupils from difficult and vulnerable backgrounds in the District.

Assistance worth 500 million shillings   was provided by the Adventist relief agency (ADRA) based in Arusha.

Munasa said that there are some unscrupulous people who have been using aid received   from donors for people in need in the community   for their benefit.

"Some even dared   to divide society on the basis inappropriate, we are very grateful  that ADRA  distributed  shoes  to  all students without knowing what background of  faith , they are from, Christian Muslim and and even those without religion  have received this help  "Munasa  said in his remarks .

He asked the citizens of the District to provide any information they see the social groups that use assistance with the objective to divide the country.
He explained that many children from poor families have been desperate to read due to lack of basic needs, including shoes.

"These shoes will help pupils in building their capacity psychologically and pupils and also will help them to   avoid getting diseases and  injuries in school, "said DC Munasa.

Referring to the support aid  ADRA Country director Dr Ngaite Nkomo said all pupil will will receive four pairs of shoes after every six months.

He said that it has been granted by Tom Shoes Company based in the U.S. through the ADRA international which is also headquartered in  the United state of America.

Dr.Nkomo said that the organization runs various projects in the education sector and explained that the agency's recently distributed 24000 books for pre-primary schools and secondary schools worth 300 million shillings.

"We believe that education is the principal method to fight against poverty and  other development challenges in the community and that is why we try to help in the development  of education sector in  every opportunity we have in the organization " She said.
ends

Saturday, April 6, 2013


A move by Tanzanian government  through the ministry of natural resources and tourism   to grab Maasai Land in Loliondo Area has sparked fear and confusion among the Maasai people who have lived in the area for many years before independence.
The ministry in what has been described as the state directives last  week  announced that it will set aside 1,500 square kilometres bordering the Serengeti National Park for a “wildlife corridor”.
According to Maasai such act will result them  be prevented from getting to their pasture land in the corridor, destroying their traditional nomadic cattle-herding lifestyle. Access will however be granted to a Dubai-based luxury hunting and safari compan
Daniel Ngoitiko, a Masai politician representing Soit Sambu ward as the Councilor in the local government an area which is part of the corridor, said the declaration amounted to an existential threat for thousands of Masai tribespeople.


 “My people’s livelihood depends on livestock for life ,” he said. “We will die if we don’t have land to graze.”
NGOs say nearly all of the Masai living in Loliondo district, where the proposed corridor will be, rely on cattle herding for food and to raise money for expenses such as school fees.
Fifty-five Masai leaders have petitioned the government against the corridor, which would place out of bounds savannah that is lush and grassy in the wet season and dusty scrubland in the dry.
They have vowed to resign their posts as local administrators at a mass rally and protest in the Loliondo town of Wasso on Tuesday. Ngoitiko, who wraps himself in the traditional bright red cloth of the Maasai, will march 20km with his constituents to the demonstration.
Ngoitiko said violence could not be ruled out if the government were to proceed. “We will fight against it until the last person is gone,” he said.
Despite the passionate resistance to the proposals, the Tanzanian government appears determined to push ahead with the proposed corridor. The minister for natural resources and tourism, Khamis Kagasheki, told one newspaper this week: “If the civic leaders want to resign, they can go ahead. There is no government in the world that can just let an area so important to conservation to be wasted away by overgrazing.”
Samwel Nangiria, government programme manager for a group of local NGOs, told  journalists visiting the Area that the Masai lifestyle, which forbids eating wild game, is harmonious with nature.
 “The government does not appreciate the way that the Masai is living with wildlife,” he said. “They’ve been using it for centuries, living with wildlife all over.”
The Masai have followed seasonal rains with their cattle across what is now northern Tanzania and southern Kenyan since pre-colonial times. But they have been gradually squeezed out of their territory. The process began in 1959 when the colonial British evicted the tribe from the Serengeti.
“My grandfather was born in the Serengeti where the national park is,” Ngoitiko said, arguing that the idea of further relocation was unacceptable. “The land we are claiming is ours because we inherited it from our parents.”
Today, of the million-plus Tanzanian Masai population, at least 66,000 live in the 4,000sq km Loliondo district. The proposed corridor will reduce their land by nearly 40%. The Loliondo highlands are nestled between two jewels of Tanzania’s tourist industry – the Serengeti National Park to the west and the Ngorongoro Conservation Area (NCA) to the south. To the east lie the salt flats of Lake Natron, while to the north is the Kenyan border.
Crucially, the reduction in land access would come at a time when climate change is already placing the tribe’s lifestyle under pressure. Jill Nicholson, programme director for local NGO the Women’s Pastoralist Council, said: “The rainy seasons are coming later and that’s putting stress on water sources.”
The highlands are crucial for the June to November dry season.
“The area which is being established in the corridor is used in the dry season grazing,” said Nangiria.
“This is the time they need it most so they can have a fallback. Another reason is the wildebeest are coming to calve in Loliondo, so the Masai have to have access to the highland to keep their cattle away from possible diseases brought by the migrating wildebeest.”
The principal hunting outfit which will be able to exploit the corridor is the Ortello Business Corporation of United Arab Emirates.
 The OBC has operated in Loliondo for 20 years, flying over high-profile clients such as Prince Andrew and the United Arab Emirates royal family on 747s which land on a private airstrip. But their clients’ wealth has not filtered down to the Masai.
Ngoitiko said the hunting lodges did not employ local people, and skirmishes had broken out between herders and OBC security.
In 2009, Masai and national police clashed after the government tried to force evictions, allegedly to allow the OBC to hunt. Ngoitiko’s younger brother Paul said he lost 50 cattle because they could not reach pasture.
 Paul remembers how losing livestock, a source of identity for Masai men, broke his father’s will. “During the morning he would ask, ‘how many livestock have died today?’ When you mentioned the number he didn’t even speak.”
Paul also claims that police burnt down his family’s bomas – homes made of mud, thatch, and cow dung. After protests, the government has allowed the people to return, but a court case is still in progress to decide their future.
The government tried to evict Masai from Loliondo again last year, but backed down after an outcry led by international advocacy group Avaaz. According to campaign director Ian Bassin “nearly a million people called on [Tanzanian president Jakaya] Kikwete to stop the evictions of the Masai. The government is responsive to global opinion.”
Kikwete has a record of dismissing the Masai lifestyle. This month, he told a group of pastoralists that “living a nomadic life is not productive”.
Paul Ngoitiko disagrees, and on Tuesday he will march with his people in protest. “We have our way of living,” he said. “Without land we cannot keep livestock, and without livestock it is a kind of death.”


Tuesday, April 2, 2013

Arusha
WACHIMBAJI 11 wa kokoto aina ya moramu wamekufa baada ya kufukiwa na
kifusi katika  mgodi eneo la Moivaro nje kidogo ya jiji la Arusha .
Hadi kufikia jana jioni maiti 9 ziliopolewa katika zoezi lililochukua
saa sita kutokana na uhaba na uduni wa vifaa vya uokoaji yakiwemo
magari ya kufukua vifusi.
Kaimu kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Arusha Kamishana msadizi
Kilongo alithibitisha kutokea kwa tukio na kusema kuwa wataendelea na
kazi ya kufukua miili yote iliyonaswa ardhini.
“Tupo hapa kuhakikisha tunaopoa miili yote ,hakuna tumaini la
kupatikana kwa watu walio hai tena”alisema Kamanda Kilongo.
Waandishi wa habari walishuhudia askari wa jeshi la wananchi kikosi
cha 977KJ wakisadiana na wananchi katika kuondoa udongo uliofukia
mgodi huo pamoja na wachimbaji.
Wananchi wa vijiji vya jirani na eneo hilo walijitokeza kwa mamia huku
vilio vya ndugu na jamaa za watu walionaswa na kifusi vikitanda na
kuleta hgali ya taharuki kubwa.
Askari polisi wakiongozwa na kamanda wa polisi wa Wilaya nao
walikuwepo katika eneo la tukio wakijaribu kuratibu tukio la uokoaji
ambalo hata hivyo halikuzaa matunda kwani hadi kufikia jana jioni
miili ya watu 11 walionaswa ilikuwa imeopolewa na hakuna hata mmoja
aliyeweza kupona.
Akizungumza na waandishi wa habari jan  katika eneo la tukio Mbunge wa
Jimbo la Arusha Godbless Lema alieleza kusikitishwa kwake na hali
ilivyokuwa katika eneo la ajali hasa kutokana na katapila la manispaa
kufika katika eneo hilo na kuishiwa mafuta muda mfupi tu baada ya
kuanza kufukua kifusi.
Lema alisema kuwa hali iliyojitokeza imeonyesha shaka ya kuwepo kwa
vifaa na vyombo vya uokoaji pindi yanapotokea majanga.
“Tunawashukuru wananchi kwa kweli wametoka wengi sana na kufanya kazi
ya uokoaji hata kwa kutumia mikono yao ila hakuna maisha tena kwa watu
waliokuwa wamenaswa na kifusi “alisema Lema katika eneo la ajali jana.
Alieleza kuwa taarifa za ajali ndani ya mgodi zilipatikana mapema sana
lakini kutokana na kutokuwepo kwa vifaa vya kisasa vya uokoaji hakuna
ambalo lingeweza kufanyika.
Kwa mujibu wa wachimbaji waliofanikiwa kukimbia baada ya kuona ngema
ya kifusi kikiangukia katika eneo la machimbo hayo  Musa hamisi na
Lokar Simon walieleza  kuwa tukio hilo lilitokea saa sita kasoro jana
mchana.
“Mimi nilianza kusikia kama vile kuna tetemeko na baadaye nikaanza
kukimbia kutoka nje ghafla nikasikia kishindo nyuma yangu sikuamini
nilichokuwa naona kwa macho “alisema
Alisema wachimbaji hao waliokufa walikuwa wakipakia moram katika
malori mawili  yaliyofika katika mgodi huo saa nne jana.
Walisema kuwa wao walisikia mtikisiko na kuamua kukimbia huku wenzao
wakiwashangaa na baadaye kujikuta wakiangukiwa na kifusi kikubwa
ambacho kilifukia hadi magari yaliyokuwa yakipakiwa moramu hiyo.
“Tumewapoteza wenzetu ,tuna majonzi makubwa sana ,tutawakumbuka
walikuwa katika harakati za kujitafutia riziki kwa ajili ya maisha yao
na familia zao”alisema Lokar.

Time Management

Translator

Popular Posts

Fellow Bloggers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews