Tuesday, April 2, 2013

Arusha
WACHIMBAJI 11 wa kokoto aina ya moramu wamekufa baada ya kufukiwa na
kifusi katika  mgodi eneo la Moivaro nje kidogo ya jiji la Arusha .
Hadi kufikia jana jioni maiti 9 ziliopolewa katika zoezi lililochukua
saa sita kutokana na uhaba na uduni wa vifaa vya uokoaji yakiwemo
magari ya kufukua vifusi.
Kaimu kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Arusha Kamishana msadizi
Kilongo alithibitisha kutokea kwa tukio na kusema kuwa wataendelea na
kazi ya kufukua miili yote iliyonaswa ardhini.
“Tupo hapa kuhakikisha tunaopoa miili yote ,hakuna tumaini la
kupatikana kwa watu walio hai tena”alisema Kamanda Kilongo.
Waandishi wa habari walishuhudia askari wa jeshi la wananchi kikosi
cha 977KJ wakisadiana na wananchi katika kuondoa udongo uliofukia
mgodi huo pamoja na wachimbaji.
Wananchi wa vijiji vya jirani na eneo hilo walijitokeza kwa mamia huku
vilio vya ndugu na jamaa za watu walionaswa na kifusi vikitanda na
kuleta hgali ya taharuki kubwa.
Askari polisi wakiongozwa na kamanda wa polisi wa Wilaya nao
walikuwepo katika eneo la tukio wakijaribu kuratibu tukio la uokoaji
ambalo hata hivyo halikuzaa matunda kwani hadi kufikia jana jioni
miili ya watu 11 walionaswa ilikuwa imeopolewa na hakuna hata mmoja
aliyeweza kupona.
Akizungumza na waandishi wa habari jan  katika eneo la tukio Mbunge wa
Jimbo la Arusha Godbless Lema alieleza kusikitishwa kwake na hali
ilivyokuwa katika eneo la ajali hasa kutokana na katapila la manispaa
kufika katika eneo hilo na kuishiwa mafuta muda mfupi tu baada ya
kuanza kufukua kifusi.
Lema alisema kuwa hali iliyojitokeza imeonyesha shaka ya kuwepo kwa
vifaa na vyombo vya uokoaji pindi yanapotokea majanga.
“Tunawashukuru wananchi kwa kweli wametoka wengi sana na kufanya kazi
ya uokoaji hata kwa kutumia mikono yao ila hakuna maisha tena kwa watu
waliokuwa wamenaswa na kifusi “alisema Lema katika eneo la ajali jana.
Alieleza kuwa taarifa za ajali ndani ya mgodi zilipatikana mapema sana
lakini kutokana na kutokuwepo kwa vifaa vya kisasa vya uokoaji hakuna
ambalo lingeweza kufanyika.
Kwa mujibu wa wachimbaji waliofanikiwa kukimbia baada ya kuona ngema
ya kifusi kikiangukia katika eneo la machimbo hayo  Musa hamisi na
Lokar Simon walieleza  kuwa tukio hilo lilitokea saa sita kasoro jana
mchana.
“Mimi nilianza kusikia kama vile kuna tetemeko na baadaye nikaanza
kukimbia kutoka nje ghafla nikasikia kishindo nyuma yangu sikuamini
nilichokuwa naona kwa macho “alisema
Alisema wachimbaji hao waliokufa walikuwa wakipakia moram katika
malori mawili  yaliyofika katika mgodi huo saa nne jana.
Walisema kuwa wao walisikia mtikisiko na kuamua kukimbia huku wenzao
wakiwashangaa na baadaye kujikuta wakiangukiwa na kifusi kikubwa
ambacho kilifukia hadi magari yaliyokuwa yakipakiwa moramu hiyo.
“Tumewapoteza wenzetu ,tuna majonzi makubwa sana ,tutawakumbuka
walikuwa katika harakati za kujitafutia riziki kwa ajili ya maisha yao
na familia zao”alisema Lokar.

0 comments:

Post a Comment

Time Management

Translator

Popular Posts

Fellow Bloggers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews