Jeshi la polisi linamsaka Mbunge wa Jimbo la Arusha Godbless
Lema kwa tuhuma za kuhusika katika vurugu zilizotokea juzi katika chuo cha
Uhasibu Mkoani Arusha na kusababisha
chuo hicho kufungwa kwa muda usiojulikana.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Arusha Kamishna
msaidizi wa Jeshi la polisi Ibrahim Kilongo aliwaaambia waandishi habari kuwa
jeshi hilo limetoa ilani kwa mbunge huyo kujisalimisha polisi haraka.
“Tunamtaka popote alipo afike mwenyewe poilisi na bado tunaendelea kumtafuta popote alipo ,ni muhimu afike tufanye naye mahojiano
kuhusu yaliyotokea katika chuo cha uhasibu ”alisema Kilongo.
Kaimu kamnda huyo alikataa kutaja majina ya wanafunzi kadhaa
waliokuwa wamekamatwa katika vurugu hizo.
“Tutawapa hayo majina ya wanafunzi tuliwakamata katika tukio
hilo baadaye kwa sasa tunaendelea kuwahoji ili kupata taarifa
muhimu za vurugu zilizotokea “alisema
Kamanda huyo kwa kifupi.
Inadaiwa kuwa Lema
anatuhumiwa kuhusika katika vurugu zilizopekea kudhalilishwa na kuzomewa kwa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.
Mara baada ya kutulizwa kwa vurugu hizo Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mgesa Mulongo aliliagiza jeshi l polisi kumkamata Mbunge huyo kwa kile kilicholezwa kuwa ni kumhusiha na
vurugu zilizotkea chuoni hapo.
Hata hivyo Mbunge huyo alikana vikali kuhusika katika vurugu
zozote na kueleza kuwa alitumia nafasi yake kuwashawishi wananfunzi kurudi
chuoni na kisha akawasiliana na Mkuu wa Mkoa kufika kuzungumza na wanafunzi
hao.
Katika tukio hilo
lililosababisha mabomu ya machozi kurindima kwa kwa muda katika viunga
vya chuo hicho Mkuu huyo wa Mkoa alijikuta akizomewa baada ya kushindwa
kuhutubia mamia ya wanafunzi baada ya kukosekana kwa kipaza sauti.
Awali wanafunzi hao walitaka kuandamana kuelekea kituo kikuu cha polisi Jijini hapa kufuatia
mwanafunzi mwenzao kuuawa katika mazingira waliyodai yana utata karibu na chuo
hicho usiku wa kuamkia siku ya jumatano
wiki hii.
Baadhi ya wananchi waliohojiwa na gazeti hilo kutoka maeneo
ya Njiro Peter Muinisi na Fredy Swat walisema kuwa wameshangazwa na hatua ya
Mkuu wa Mkoa kumnyooshea Lema kidole na kuagiza akamatwe kuhusiana na tukio
hilo.
“Hii ni aibu tulimwona Lema akiwabembeleza wanafunzi
wasiandamane kwenda kati kati ya
mji ,alitaka jambo hilo litafutiwe
ufumbuzi bila kuleta madhara yoyote,hebu fikiri wanafunzi wale wangefika kati
kati ya mji hali ingekuwaje”alihoji Muinisi.
Aidha alisema viongozi wanapaswa kuheshimiana na kutenda
kazi bila kuweka sababu za kibinafsi katika mambo ambayo majibu yake yako wazi
mbele ya umma na kutengeneza picha mbaya kwa viongozi.
0 comments:
Post a Comment