Sunday, April 14, 2013


Mfanyabiashara Maarufu Mkoani Arusha Peter Joseph Mallya almaarufu Bob Sambeke amefariki dunia baada ya kuanguka na ndege yake binafsi muda mfupi kabla ya kutua katika uwanja mdogo wa ndege uliopo katika eneo la Magereza kilomita sita kutoka kati kati ya Jijiji la Arusha.

Kaimu kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Arusha kamishna msaidizi wa Polisi Ibrahim Kilongo alisema kuwa ajali jiyo ilitokea saa moja na nusu jioni.

Alisema kuwa marehemu Mallya alikuwa peke yake na ndiye amepoteza maisha na kuacha ndege hiyo ikiwa imeharibika vibaya kutokana na kuangukia miti mikubwa iliyokuwa katika eneo la ajali.

“Ni kweli ajali imetokea na tayari mwili wa marehemu upo katika chumba cha kuhifadhi maiti ukisubiri taratibu za familia yake za mazishi”alisema Kilongo.

Alisema kuwa chanzo kamili cha jail hiyo bado hakijafahamika na kwamba uchunguzi utaendeshwa na vyombo vya usalama na mambo ya anga ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Hata hivyo habari ambazo bado hazijathibitishwa kutoka kwa maafisa wa mtandao wa kuongozea ndege uwanjani hapo zinasema kuwa marehemu alikatazwa kutua na ndege yake katika wakati huo lakini haifahamiki ni kwanini hakufuata ushauri huo.

Ajali  hiyo ni ya pili kutokea karibu na uwanja huo baada ya mwaka 1998 kutokea kwa ajali ambayo iliua watu sita baada ya ndege ndogo aina ya cesna kuanguka kati kati ya shamba la kahawa katika eneo hilo.
0 comments:

Post a Comment

Time Management

Translator

Popular Posts

Follow by Email

Fellow Bloggers

Google+ Followers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews