Wednesday, October 31, 2012

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kesho anatarajiwa kuzindua hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha vijijini Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.

Hospitali hiyo  ya Olturumet iliyopo katika kata ya Olturumet  inatarajiwa kutoa huduma kwa wakazi  zaidi ya laki tatu wa halmashauri hiyo ambayo haikuwa na hospitali baada ya kuundwa kwa halamashauri ya Meru ambayo ilichukua hospitali ya Wilaya iliyokuwaepo ya West Meru.

Akizungumza na Blog hii Mkurugenzi wa Halmashauri  hiyo Halifa Ida alisema kuwa hospitali hiyo pia itahudumia wananchi wa kata na vijiji vya jirani kutoka  Wilaya ya Longido itakuwa na vitanda vya kualza wagonjwa 115.
Alisema kuwa hospitali hiyo  imejengwa na serikali kupitia miradi yake ikiwemo mradi wa maendeleo ya afya ya msingi ,mradi wa maendeleo ya jamii (TASAF) nguvu za wananchi na wahisani kutoka nchi za ujerumani na Marekani.
“Hawa wadau wa nje  ambao ni Shirika la umoja wa madaktari wa ujerumani  walitusaidia kujenga wadi ya  upasuaji, na wodi nyingineya wanaume hakika wametusogeza kufikia hapa tulipofika”alisema Hida.
Hida alieleza kuwa hadi kufikia hatua ya kuzinduliwa ujenzi wa wadi ,maabara ,vyumba vya upasuaji na vipimo mbalimbali gharama zake zinafikia zaidi ya shilingi milioni mia sita.

  Alileza kuwa hopitali  hiyo itasaidia kutoa huduma ya mama na mtoto hasa wanawake wajawazito wa Wilaya hiyo ambao  wanakatishwa maisha yao  kutokana na kujifungulia majumbani kufuatia  uhaba wa huduma za afya.

’Ni jambo la faraja sana kwa watu wa jamii za kifugaji kusogezewa huduma za uhakika za afya ,hospitali hii itachochea ustawi wa maisha ya jamii hii”alisema Hida.

Rais Kikwete pia anatarajiwa kuzindua Halmashauri ya Jiji rasmi baada ya mji wa Arusha kupewa hadhi hiyo kisheria mwezi Agosti mwaka huu,kuzindua chuo kikuu cha Nelson Mandela  na baadaye kuhutubia wananchi wa Jiji la Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini humo.

0 comments:

Post a Comment

Time Management

Translator

Popular Posts

Blog Archive

Fellow Bloggers

Popular Posts

Visitors Worldwide

Total Pageviews